Mke wa mchuchu yuko busy kunitafutia mume - imekaaje hii

1.pasaka usihudhurie huko ulipoalikwa.
2.acha mawasiliano na mke wa mchuchu.
3.badili saloon.
4.badilii namba.
5.habari ya petro achana nayo ,km ni mume utapata tu mwingine (Reason;hauwezi kuwa uhusiano wenye manufaa na kuaminiana)
6.mchuchu wako endelea naye tu mpaka utakapopata wako au akuongeze mke wa pili.
 
olewa haraka kama utampenda Petro, Mhina mtakuwa mnakumbushia tu.

mwachea endelee na mhina hadi nyama za mashavu zitakapoporomoka na mikunyanzi itakapozidi, atamtafuta mr mhina hatomuona, maana mhina atakuwa ubavuni mwa mrs mhina..... Ndipo atakapotamani angemkubali petro.......
 
Kumbe ndio MABUZI yanavoitwa siku hizi i.e. MCHUCHU.

Mchuchu ni la zamani zaidi kuliko hilo buzi. Mimi nakumbuka tangu miaka ya sitini lakini lilipotea na sasa hivi limeanza kurudi tena.
 
unafurahia kabsaa kuwa nyumba ndogo! ama kweli ule usemi kwamba mwalim wenu kipofu wewe umeutimiza
 
Mbona huridhiki? umekuwa ukitoka na bosi wako yaani mume wa dada yako leo hii tena na mume wa mtu tena huwa anakufuata hapo ofisini kwenu, huoni aibu? hadi mfanyakazi mwenzio huyo muhaya anakushangaa. achana na mume wa watu bana kuna vijana fresh hawajaoa utapata. ila sishangai mabinti wa kichaga mpo hivyo. utarogwa huyo mama katumia ustaarabu kufanya hivyo. utajuta ukiendeleza ubishi.
 
Wewe au rafiki. Acha mume wa mtu. Mtafute wako, tulia kwanza kama petro ni wako atakuja muda muafaka. Kama mumeo akiibiwa utapenda?
haaa apende wap? tena mtu wa dizain hii akiibiwa wake anawehuka km mbwa aliekosa chanjo
 
yani wewe useme mme wangu mimi anakuweka mjini walah siku nikikugundua nakumaliza...unajitamba na vya wenzako hata haya huna!looooh
 
Cha kufanya we hamua kuwa na huyo petro achana na mume wa mtu,chukua chako,huyo mhina hawezi kuwa wako.
Nb "mume wa mtu ni sumu" watch out
 
Tobaaaaaa kumbe unamjua kiundani hivyo? Pole yake,

ila na wewe tafadhali sana futa hiyo kauli yako ya 'mabinti wa kichaga mpo hivyo' sio wote bana wengine tumezaliwa kwenye familia zenye maadili na hofu ya Mungu japo ni za wachaga pia... Hiyo ni tabia yake yeye mwenyewe na sio tabia ya mabinti wote wa kichaga..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…