Mke wa mshikaji wangu aniduwaza!

wamogori

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
888
Reaction score
339
Jana nimeduwazwa sana baada ya mke wa rafiki yangu kunitamkia wazi kuwa ananipenda na anataka kutoka na mimi.
Tangu nifahamiane naye miaka takribani mitano sasa tumekuwa tukiheshimiana naye sana kama mashemeji. mwaka huu akaniambia kuwa mumewe ameanza kubadilika kwa kuzidisha ulevi, kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kulala nje na pia alizifuma meseji za mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa mtu aliyemsave kwa jina la kiume, hivyo nimsaidie kumshauri ili abadilke ila akanionya nisimwambie kama ni yeye ndiye kaniambia.

Nilimtia moyo kuhusu hali hiyo na kumwomba awe mvumilivu na asichoke kuongea na mumewe kuhusu hali hiyo ili abadilike. Binafsi nilipata wakati mgumu wa namna gani nitamshauri jamaa bila kumtajia makosa yake na wapi nimeyapata hivyo nikashindwa hiyo kazi.

Mke wa jamaa akaanza kunipigia simu usiku kulalamika kila mumewe anapochelewa kurudi na wakati mwingine akinipigia alfajiri kuniambia kuwa mumewe hajarudi hadi muda huo. Niliendelea kumtia moyo ingawa mambo hayo yalikuwa ni ya kweli.

Cha ajabu kuanzia wiki jana amekuwa akinitumia meseji za mapenzi, nikajua ni hizi meseji ambazo watu hutumiana hivyo sikujali sana hadi pale aliponiandikia akiniambia kuwa yuko serious anataka kutoka na mimi. Sikuamini nikampigia simu kusikia sauti yake kama ni yeye kweli, ndipo aliponithibitishia kuwa yuko serious na atatunza siri na kunitunzia heshima yangu kwa jamaa kwani tayari moyo wake umeangukia kwangu.

Sikuweza kumjibu kitu kwa namna nilivyopatwa na mshangao. hadi sasa anaendelea kunibembeleza na kunipa mbinu nyingi za kutimiza lengo lake bila kujulikana na watu.

Binafsi sina lengo la kumsaliti mshikaji wangu ila nimelileta kwenu ili mnishauri nimjibu vipi huyu mwanamke ili heshima yangu kwa familia hii iendelee kuwapo na pia kusitokee chuki yoyote kutokana na kadhia hii itakayopelekea urafiki wangu na familia hii kuyumba au kupotea.
 
Mkuu,pepo la ngono likimwingia mtu huwa lina nguvu sana.Sina mengi ya kukusahuri ila acha kabisa,huyo mwanamke amezidiwa na hilo pepo.Kumbuka hata wanaoshikwa ugoni huwa wanaanza kwa siri lakini huwa wanakamatwa.Yangu ni hayo tu.
 
Kikulacho ki nguoni mwako!!!!!!!!!! Wewe una Mke au ndo senior bachelor?

Dawa yake moja tu huyo muignore usimpigie, usipokee simu yake wala kujibu text zake.

Hizi ndoa za siku hizi MAJANGA! Nikisema either way LIFE FU.CKS YOU!!!!!!! Naonekana mbaya! Ona sasa jamaa aliona kuoa ni suluhisho kumbe my wife anatembezea washkaji zake Kabang bila haya!!!!!!!!!!! Chinekeeeeeeeeeee! Heeeeeey!
 
Sio kama kakupenda anachofanya anataka kulipa kisasi kwa mumewe kutembea na rafiki yake mmewe(wewe) hayo sio mapenzi ni maamuzi ya kisasi tu.
usifanye huo upuuzi utakuja kujuta rafiki yangu.
 
...Vunja mawasiliano na jamaa yako pamoja na mkewake....Huko mbeleni jamaa atajishtukia kwamba tabia yake ya ulevi imemfanya rafiki zake wamzarau pia huyo mkewe ukimkatia digitali.. atajihisi aibu...na mwisho atarudi sambamba kwa mumewe ambaye tayari atakuwa anarudi kwenye stari wa mwazo!!!

...ukiipuuza ushauri niliokupa hapo juu ....tambua kwamba kugugudelo halina macho linatumia sikio na macho kuona...
 
Mtoke mwende wapi? Ka mkienda nae kanisani kunaubaya gani?
 

Kweli kaka!!!....
 
Mwanamke laanakhuum
Kimbia ndg huyo ni mbaya kama
ukoma vile,ukila nyama ya mtu
huwezi kuacha.
 

ahha dnt twist the story bwana...sasa mambo ya kabang umeyatoa wapi...plus this guy had it coming...u got to treat ir wife well bwana mpaka mwanamke atoke nje ndugu yangu mume kafanya kitu kibaya sana...wanawake wavumilivu sana na kwambia mpama mke atoke ujue in most cases mume amemtenda vibaya
 
Sasaa unashangaa nini? Hujaelewa somo au unaturingishia kupendwa na used?

Konnie please! Is that the only asset which remained in your stock of MEDULA OBLANGATA? Huyu mleta mada yamempata ya kumpata bhana ps msaidie
 
af mbn kama unasikilizia utamu vile!!!
NIMESEMA tu!
 
Sio kama kakupenda anachofanya anataka kulipa kisasi kwa mumewe kutembea na rafiki yake mmewe(wewe) hayo sio mapenzi ni maamuzi ya kisasi tu.
usifanye huo upuuzi utakuja kujuta rafiki yangu.

Tell him!!!!.....
 
vizuri kama hutami kumsaliti jamaa...wee panga kuongea nae face to face na make r stand clear in no uncertain terms kuwa hilo haliwezekani....nothing gud has ever come out of affairs.

Kwa nini JF watu wameanza kuiba Password za wenzao?
Hili jambo halikubaliki hata kidogo...Mzabzab...!! haiwezekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…