Mke wa mtu anadai mtoto aliyezaa kwenye ndoa ni wangu

Captain Phillip

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
894
Reaction score
538
Kwanza nianze kwa kuwasalimia Great Thinkers na naamini mtanipa ushauri wa Hekima na Busara.

Mimi ni kudume ambaye kwa sasa nina mke na watoto watatu kwa ufupi niko kwenye ndoa huu mwaka wa 6.Kabla ya kuwa na mke niliye naye nilikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine kwa muda wa miaka 6 na hatukuendelea na uhusiano si kwa sababu nyingine bali ni haraka yake ya kutaka kuolewa kipindi nikiwa bado masomoni.So aliniuliza kama niko tayari kumuoa na kweli sikuwa tayari so akaamua kuolewa na mwanamume mwingine.

Nilirudi nyumbani kwa ajili ya likizo nikakuta tayari ameshaolewa na ana takribani miezi miwili kwenye ndoa but aliposikia nimerudi alinitafuta na akadai kuwa mwanamume aliyenaye hampi shughuli kama aliyokuwa akipata toka kwangu hivyo nikajikuta tumeduu hivyo hivyo.Hiyo ilikuwa ni mara moja tu na hatukuwahi kurudia tena manake na mimi nilikaa muda mfupi tu nikawa nimeoa.

sasa Ishu ilianza kipindi huyu mpenzi wa zamani akiwa mjamzito coz aliniambia kuwa huo mzigo ni wangu na alinitegeshea kwa makusudi ila nilipuuzia kwa kuamini zilikuwa ni stori za kujifurahisha lakini hali imekuwa mbaya zaidi hivi majuzi baada ya yeye kurudi kijijini kwetu akiwa na mtoto wake huyo mwenye miaka 8 kwa sasa kwani ni carbon copy yangu na hata mama yangu mzazi alipomuona alinipigia simu na kuniambia hilo hilo kwani akisimama na mwanange mwenye miaka 6 kwa sasa ni kama mapacha.

Nifanyeje sasa na kila mara anapigia simu kuniambia kuwa binti yako anakusalimia na mwenyewe nilipomwona nikataka kuzimia coz ananifanana koprait.
 
walimwengu hawaishi vituko...........
je yeye anataka umchukue mtoto?
na mumewe anajua kwamba mtoto sio wake?
 
Hahahahahah pole sana kaka ishini no kwa akili ndio hiyo hapo
sasa suala la huyo binti yako sijui ,nakusalimia tu
 
Kitanda hakizai haramu ndugu yangu, mchukuwe tu mwanao
 
Naomba mungu yasije nitoke haya. mke wangu anaweza kunichinja aisee, hiyo ni nomaaaaaaaaaaa! Mtoto wa nje kwa sisi wanaume ni zaidi ya mateso, na ukkuta huyo mama mtu akili zake ni za kwenye kiroba, utajuta kwa nini umeoa, maana utapigishwa kwata mpaka ukome.
 
usije ukajidanganya ukamchuka huyo mtoto wewe na huyo mwanamke mtapoteza ramani na raha ya maisha.wewe utakabiliwa na msalaba wa wife wako na huyo mama mtoto ata achika wakati huwezi kuwa nae tena kwa amani.potezea mtoto ni wa baba mlezi kama ni kweli
 
Siku zote kila mla cha mwenzie na chake huliwa!
Ww jiandae na ww kulea watoto wasio kuwa wako!
Sipendi wanaume wazinzi,na waizi wa wake za watu.
 
wewe unachohitaji kutoka kwetu nii hasa???
 
hiyo siyo issue,
karibia kila nyumba ina watoto kama hao,
mwambie mama yako amwambie dada akae kimya
aendelee kumlea mtoto, angalia sana ili asome vizuri.
 
kwa hiyo wewe low thinker, unataka tufanyeje sisi great thinkers....!!???
 
huyo mwanamke c mzima. Amezaa kwenye ndoa? Mumewe anajua mtoto ni wake? Kwa nini akufuate hata kama kweli mtoto ni wako. Kuwa mwangalifu mume wa mwenzio atakuchinja. Msala huo
 
Mtoto ni wa yule anayemlea na si wa yule aliyempa mimba, fatherly love kwa mtoto huwa ni ya yule aliyemlea si ya yule aliyetoa mbegu kwa scenario hii. Maana kina baba wengi sana wanalea watoto wasio wao na still wanapendwa na wanakuja kutunzwa na watoto hao hao. Sana sana huwa life stress ya yule anayejua mtoto ni wake i hali si wake. Kama ndugu yetu huyu, mama yake na huyo malaya na hiyo wataiwaza mpaka kaburini kwao na hawatakuwa na right ya kumchukua mtoto.
 
Sasa unataka ushauri gani wakati unajua mtoto ni wako na mwenyewe uliridhia kutembea na mke wa mwenzio?Amua kama una ujasiri wa kumweleza mkeo kabla siku moja hujarudi nyumbani na kukuta binti na mkeo wanakusubiria sebuleni.
Alafu jua kwamba yawezekana na wewe unaolea sio wako, maana kila mwosha huoshwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…