Mke wa mtu

Kifuniko

Member
Joined
May 20, 2011
Posts
97
Reaction score
18
Mimi niko nje ya nyumbani(TZ) niko ugenini, kazini kwangu kuna dada wa miaka kati ya 24-30 ni mfanyakazi mwenzangu na ni mke wa mfanyakazi mwenzetu, ananitaka kwa nguvu ametumia email ameona kimya sasahivi amehamia kunitafuta kwa simu mimi sipokei wala kujibu ujumbe , naombeni ushauri maana ni kero kwangu, je nimweleze mumewe?
 

Hapana, usimweleze mumewe. Mkanye yeye mwenyewe na mwambie akuache na aiheshimu ndoa yake na amheshimu mumeme na kwamba wewe huna raghba naye.

Good grief....this is not rocket science.
 
nimeshamweleza sana kwa mdomo kwani sitaki ushahidi wowote wa ujumbe wala kumpigia simu lakini hanielewi
 
Hahahaaaa....kama kweli umemweleza lakini bado hakuelewi basi hukuwa serious katika maelezo yako.

ukitaka kujua ukweli wa hii habari...
mwambie akuelekeze huyo mwanamke,ikiwezekana akupe namba ya simu ya huyo mwanamke
..lol
 
Nawe ni mume wa mtu??
Kama na we ni mume wa mtu, hakuna tatizo kwakuwa wote ni wezi.
Pia, kwanini ukubali kuishi kwa tabu, mwaleze kuwa haumtaki, huo ndio uanaume.
 
Mpe anachokitaka... Kwa nini aumie kwa ajili yako? Hapa duniani tunapita tu bro!
 
Kucheza na nyumba za watu ni sawasawa na kucheza moto!
 
Mpe anachokitaka... Kwa nini aumie kwa ajili yako? Hapa duniani tunapita tu bro!

ogopa sana mke wa mtu! Nimeshuhudia jamaa akiwa kachinjwa kama kuku na kichwa chake kucharangwa kama kitimoto. Jamaa alifumaniwa na mke wa mtu porini wakipeana majamboz. Nilitamani kukimbia,ila sabb ya kaz ya wito ilibidi nivumilie!
 
nimeshamweleza sana kwa mdomo kwani sitaki ushahidi wowote wa ujumbe wala kumpigia simu lakini hanielewi

Mbona bahati hizi huwa hazipiti upande wangu! nimemkosea nini mungu?
 
Kwanini usiwe kama bob marley. Mpe mwenzio kitu mungu amekupa bure, siamini kabisa kuwa huitaki hata mara moja kwakuwa haiishi.
 
huyo mwanamke ni raia wa hiyo nchi?nawe makaratasi yamekaa vizuri?angalia babu,usije chezea shilingi karibu na shimo la choo!
 
mpe vesi:"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi. Hatakubali ukombozi uwao wote; Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi. " (Mithali 6:32-35).
 
jiepushe naye mkuu
kaa mbali naye kwa nguvu zako zote
mwambie kuwa utamwambia mumewe
 
nafikiri wewe unataka kifo mapema kumkaribia mke wa mtu tena na mikosi wala nionavyo huna malengo ktkt maisha yako unabaki kuangalia wake zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…