Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Hatua yake hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamikia uamuzi wa Bunge kumuongezea posho na kufikia Dola 3,500 kwa mwezi, kama ilivyotokea pia kwa mke wa Makamu wa rais, kwa madai kwamba wamekuwa wakifanya kazi kubwa nyuma ya viongozi hao.
Kwa mujibu wa Rebecca, ameamua kurejesha Dola 151,618, jumla ya kiasi cha fedha alichokusanya kama posho tangu mumewe awe rais miaka minne iliyopita.
Akifafanua juu ya uamuzi huo, amesema amejisikia vibaya kwa namna watu walivyokosoa hatua ya Bunge kuwaongezea posho yeye na mke wa Makamu wa Rais, hivyo anataka kuilinda taswira yake.