Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Familia imenogewa na kiti cha Urais baada ya Mume sasa Mke naye akitamani kiti hicho!
===================
Mke wa Rais wa zamani wa Ivory Coast, Simone Ehivet Gbagbo ametangaza kuwa atagombea katika Uchaguzi wa Urais wa 2025, akisisitiza kwamba anataka kuijenga Ivory Coast mpya.
Amesema kuwa alikubali kuwa mgombea wa uchaguzi wa Urais mnamo Oktoba 2025 kwa sababu anaamini sana kwamba kila raia wa Ivory Coast, bila kujali hali yake, ana uwezo, ikiwa kweli wanataka kuvuka kila aina ya changamoto za kuota, kuunda, kujenga na kufanikiwa,” alitangaza Bi Gbagbo.
Wagombea wengine watatu wanaowania urais utakaofanyika Oktoba 2025 ni Rais wa zamani (na mume wa zamani wa Simone Gbagbo) Laurent Gbagbo, Waziri Mkuu wa zamani Pascal Affi N’Guessan na Waziri wa zamani wa Biashara Jean-Louis Billon.
Rais Alassane Ouattara bado hajaeleza iwapo ana nia ya kuwania muhula wa nne au la.
Simone Gbagbo (75), alikuwa mke wa Rais Laurent Gbagbo akiwa madarakani kutoka 2000 hadi 2011, ambapo wakati huo alipewa jina la utani la Iron Lady.