khamis kilo
JF-Expert Member
- May 23, 2016
- 1,137
- 1,380
Ngoja niende moja kwa moja kweye mada husika, jana mida ya saa 10 jioni nilipokea simu kutoka kwa bi mkubwa mmoja wa makamo kidogo miaka kama 55 hivi, huyu bi mkubwa alikuwaga jirani yangu nilipokuwa nimepanga mwanzo na mpenzi wangu.
Baada ya kupokea simu yake alianza kujitambulisha mimi ni mama X hapa jirani yako ulipohama, samahani mwanangu naomba tuonane kuna jambo muhimu sana, nikamjibu sawa mama ila saa hz natoka kazini nikifika nyumbani nitakuja huko kwako akajibu sawa naomba uje usikose nakuomba sana, nikamjibu sawa hakuna shida. Niliitikia wito wa kwenda bila kujua kuna jambo gani limetokea.
Sasa wakati nimerudi nipo nyumbani napata chakula mke wangu yupo pembeni nilimuona akiwa kwenye mawazo sana hadi nikamuuliza unawaza nini?, alichonijibu akasema “hamna siwazi kitu”…nilipomaliza kula nikamuuliza tena una shida gani mbona leo umepooza sana, ndio akaanza kuniambia kuwa kuna jambo limetokea ila anaogopa kuniambia, nikamwambia niambie tu hakuna shida, akaanza kufunguka akitanguliza msamaha kwanza “samahani sana naomba unisamehe huku akilia” nikamwambia niambie kuna nini, akaanza kulia tena nisamehe hamy eti mama X amekuta msj zangu kwenye simu ya mume wake msj ambazo ni za muda sana nilikuwa nachat na mume wake ndio kaziona leo. Kiukweli nilipata presha kidogo nikasema okay hakuna shida, mimi nitaenda huko kwa mama X kuona hizo msj.
Nikampigia yule bi mkubwa nikamwambia mama ndio nakuja huko kwako nikukute akasema sawa, nilipofika kwa yule bi mkubwa akaniambia “mwanangu samahani sana kitendo alichokuwa ananifanyia mke wako ni kibaya sana, hapa nilipo hata sijui nifanye nini?, ila nitamfanya kitu kibaya mke wako”, aisee nilishtuka sana nikamwambia kuna nini?, ndio bi mkubwa akanipa simu akiniambia angalia hizo msj za mke wako alivyokuwa wanawasiliana na mume wangu. Daaah nilikuta msj za hovyo sana tena sana wanawasiliana mara wakutane gest wanayoendaga, mara wakafanye mapenzi kwenye jumba, mara vichochoroni, mara chumbani kwake yaan mzee alikuwa anavizia mke wake akiwa hayupo anamuingiza mke wangu chumbani kwake anaenda kula tunda, mara chooni yaan msj kibao za hovyo, wakati nasoma zile msj yule bi mkubwa alikuwa akilia hadi baadhi ya majirani wa pale wakaja na wao wajue nini kinaendelea ndio bi mkubwa akaanza nae kufunguka “yaan huyu mtoto ambae ni mke wangu, lazima nimfanye kitu haiwezekani kabisa atembee na mume wangu alafu aniache mimi hapa nateseka na familia”, ndio majirani nao wakaanza kufungua, mbona sisi tulikuwa tunajua hayo mambo lakn tulikuwa tunaogopa kuongea maana tungesababisha mauaji, nikasema okay mama hakuna shida.
Nikaondoka zangu wakati nipo njiani nilikuwa na hasira sana, nilipofika nyumbani nikamkuta mke wangu analia sanaa huku amesika kisu bora nijiue mimi nitaenda wapi sasa, nisamehe mume wangu nimekosa nisamehe sana, aisee tukaanza mikimiki pale ya kumpokonya kisu kwanza kabla ya mambo mengi, nikabahatika kumpokonya kisu huku bahati mbaya kikiwa kimemkata mkononi damu kama zote, sasa wakati nilipokuwa kwenye harakati za kumpokonya kisu kumbe nje majirani walikuwa wanasikia zile kelele zake ndipo majirani nao wakaja ili wajue kuna nini, kufika pale wanakuta damu kama zote huku mm nikiwa nimeshika kisu mkononi, mke wangu yupo chini analia “naomba unisamehe hammy nisamehe mimi nitajiua usiponisamehe”, yaan hadi naandika haya sijui hata nimfanye nini huyu mwanamke [emoji51]…..?