Nimeanza kuishi na huyu mwanamke toka mwaka 2007 wakati huo tulikuwa tunaishi kama wapenzi na tulikuwa tunatembeleana tu yeye akiwa Dar na mimi nikiwa nafanyakazi Mbamba Bay lkn ilipofika mwezi Desemba 2009 niliamua nipeleke barua kwao ili nioe,jambo la ajaabu lililotokea nilitajiwa mahali kubwa sana yaani Tshs 4,500,000/= mimi nilkawa nimeshindwa kuilipa na ndoa ikashindikana na yeye akarudi kwao Arusha, niliumia sana kwa kukosa kumuoa ilipofika mwezi Machi 2010 yeye alinipigia simu na kunieleza kuwa yuko tayari kuja kuishi na mimi Mbamba Bay ingawa wazazi wake walinitajia mahali kubwa,nilikubali kumpokea na kweli alifika.
Maisha yetu yalikuwa mazuri sana na kila mmoja wetu alisahau tofauti zilizotokea, lkn baada ya kama mwezi mmoja alianzisha ugomvi ambao tulishindwa kuusuluhisha na aliomba nauli ya kurudi kwao na nilimpa.
Ilipofika mwezi Juni 2010 aliomba radhi na akaniomba tuishi tena na mimi bila kinyongo nilikubali ila moyo wangu ulikuwa na wasiwasi kidogo nikaona kuwa safari hii atakapokuja basi ni lazima tucheki HIV.Nikikwenda kumpokea Mbeya na alipofika tu nilimweleza kusudio langu la kupima HIV mimi na yeye .Tarehe 6 Julai tukaenda kupima pale Hospitali ya Rufaa matokeo yake yeye akawa amekutwa na Virusi vya UKIMWI na mimi nikawa sina! Tulipewa maelekezo ya jinsi gani ya kuishi katika mahusiano yetu.Mwenzangu aliipokea hali yake kwa majonzi na mimi nikawa na kazi ya ziada kumtuliza,tukarudi wote Mbamba Bay ila baada ya kurudi tu kama wiki mbili akanywa sumu ili afe,tulimuwahisha Hospitali na tukafanikiwa kuokoa maisha yake,lkn ghafla akanijengea chuki ambayo haina mfano na aliahidi mbele yangu kuwa ni lazima aniue! Niliwaelezea wazazi wangu na wazazi wake pia,wazazi wangu wakanishauri nimrudishe kwao na mke wangu akawa hataki kurudi kwao na tuliendelea kuishi hivyo hadi mwezi Oktoba tarehe 16 alipoamua kuondoka mwenyewe.Ingawa mke wangu ameondoka bado nampenda ila nilipokuja kufanya uchunguzi zaidi nimekuja kufahamu kuwa maisha yake yalikuwa ni ya kutangatanga sana na hivi sasa yupo Dar! Nifanyeje?

Ninapata faraja kubwa kwa haya yote mnayonishauri,kumbe mtu ukiwa na tatizo uka-share na wenzako kwa namna moja unapata unafuu moyo unatulia na akili pia inatulia nawashukuru wote tena kwa moyo mmoja,ila kwa muda huu sina mpango wa kutafuta mwanamke wa kuoa ni mapema mno na nimepata funzo kuwa ndoa siyo jambo la kukurupuka!
mkuu kumbe wa kunyumba kabisa "CHIMKO"Wana JF ninawashukuru kwa mawazo yenu na ushauri,ni kweli ndoa kati yangu na huyo dada wa KINYIRAMBA haikuwahi kufungwa kwa kuwa mimi nilishindwa kulipa MAHALI ya Tshs 4,500,000/= labda wakwe zangu hawakutaka kunioza mtoto wao,mimi kwa Kabila ni MMAKUA,ila tukija kwenye utaratibu mwinginene ni kuwa tumeishi pamoja zaidi ya miaka miwili hivyo naweza kusema ni mke kwa kuzingatia jambo hilo.Waungwana napenda ni washukuru tena na msichoke kuniombea ili nibaki NEGATIVE,kwa upande wa dini mi ni Muislamu na tayari nilishaweka ahadi kuwa nikipima mara ya pili na kuonekana niko salama nimtolee MWENYEZI MUNGU SWADAKA,na tayari nimeshafanya hivyo.
Ndiyo mkuu "KINON'KOLELA"mkuu kumbe wa kunyumba kabisa "CHIMKO"