Mke wangu ana lalamika matiti yanauma mno msaada kwa wataalamu plz.

Mke wangu ana lalamika matiti yanauma mno msaada kwa wataalamu plz.

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,750
Reaction score
2,283
Mke wangu ananyonyesha mtoto mdogo wa miezi mitatu sasa! Lakini amekuwa akipatwa natatizo ambolo hata sielewi ndo ugonjwa gani! Amekuwa akiumwa na matiti yani yanavimba halafu yanauma ukigusa tu anapiga kelele na maziwa yanagoma kutoka, yani anakesha analia yakianza kuuma, hospital nilimpeleka dakitari akanipa vidonge vya kutumia tu huku akinipa ushauri ambao eti ni kawaida kwa wamama mtoto akimcheulia kwenye nyonyo huwa maziwa yanauma hivo! Naomba msaada wenu hasa kujua kwa wamama pamoja na madakitari hali hii ni kawaida au ni tatizo linalosababishwa na nini mi nawaza zisije kuwa dalili za kansa ya ziwa naogopa sana aisee!!
 
Mwanzo yanauma Lakini sio mpaka mieZi mitatu, mie Nilikua na tatizo Hilo Lakini mwezi wa kwanza nilipo kufungua, maziwa yakawa hayatoki, bibi akanisagia , uwatu, asali, pili pili manga, samli fresh, na vitu nyengine nime sahau.. Anasaga kila asubuhi unakula kikombe 1 cha kahawa kabla hujala chochote Lakini inataka moyo , inasafisha tumbo maziwa ndio yatatoka Lakini Hilo joto lake mwilini unaweza kusema unahoma....
 
shemeji atakua hamyonyeshi vizuri mtoto ,aongeze jitihada za kumnyinyesha,pia azingatie ushauri wa daktari!
 
hilo jambo hutokea hapo awe anakanda hilo titi kwa maji ya uvuguvugu hata mara tatu kwa siku upunguza maumivu na kupona kabisa.
 
Au na wewe huwa unamnyonya mkuu?
 
pole mkuu hata mpenzi wangu analo hilo tatizo ila yeye humtokea akikaribia cku zake lakini baada ya hapo maumivu hupotea kwahiyo hiyo ni hali ya kawaida na itaisha mkuu usijari
 
Back
Top Bottom