Wazazi wa zamani kwa namna moja ama nyengine walikuwa sahihi sana kutafutia watoto wao wake/waume wa kuoa maana waliangalia mengi,,familia atokayo kijana,magonjwa ya kurithi etc,sasa hawa watu wa kukutana nao tu nyiani then mnacopy na kupaste ndo matatizo yenyewe hayo sasa!duh hatariiiiiiiiiiiiiii
Hapo kuna kazi!Ila labda nyumbani mume anakua mkorofi na kiburi sana so inabidi aweke mambo live..ili angalau huyo mwanaume aone aibu kidogo!Upande wa pili wa habari unahusu sana hapa...kama huko nyumbani hasikilizi mama wa watu afanyeje?
:angry: "Kijana amekumbwa na Mkasa, Mke wake alianza na Kumtuma Baba mkwe aje kwa mume wake waongee matatizo ya Ugomvi wao, bila hata taarifa. Unafungua ofisi unaenda kwa bossi unarudi unakuta baba mkwe amekaa mezani kwako toka Mkoani na begi. Baada ya hapo Mke nae amegeuza ofisi ndio sehemu ya kusuluhisha matatizo ya Nyumbani.
"Dunia ina Mengi"
Hahaaaa jamani nacheka kama mazuri, hilo linaitwa sokomoko na tedi. Hee au timbwili la asha ngedere, mh baba mkwe na begi ofisini? Makubwa ndo tabu yakuoa familia zisizo na maadili. Sasa kama mzazi hatna hekima then wewe utaenda kushtaki wapi, mh hakuna ndoa hapo. Ni uswahili fuulu.
good one sis' tatizo hizi ndoa za mjini huwa tunaokotana tukabla ya kufunga ndoa ni vyema ujue uwezo wa mwenzio wa kuvumilia mambo magumu, ufahamu wa jumla, kuchanganua mambo na uwezo wake wa kufanya maamuzi.
Baba na mwanawe wote ni mapoyoyo wa kutupwa
Ugomvi baina ya wanadoa ni kitu cha kawaida....
Mwisho wa yote watakuja kupatana warudie mapenzi yao matamu kama zamani wawaache watu wakijuliza " imekuwa vipi?"
Ndoa zote hupitia magumu lakini kuna siku shetani au kidudu mtu atashindwa kwa jina la yule aliye juu ya yote na wote.
Mke anayemfuata mume hadi ofisini huyo amekosa maarifa na subira tu.Aelekezwe kuvumilia kuna siku uvumilivu utalipa.Watu huvumilia hata miaka 20 ndivyo ndoa zilivyo, na katika kipindi hicho kuna mapito mengi ikiwemo vishawishi vya kila aina.Wengine hutafuta talaka kwa hali zote, wengine hupata wapenzi wapya, wengine kufanya fujo na kuonekana kituko mbele za jamii....YOTE YANA MWISHO MRADI UVUMILIVU.
Wazazi wa zamani kwa namna moja ama nyengine walikuwa sahihi sana kutafutia watoto wao wake/waume wa kuoa maana waliangalia mengi,,familia atokayo kijana,magonjwa ya kurithi etc,sasa hawa watu wa kukutana nao tu nyiani then mnacopy na kupaste ndo matatizo yenyewe hayo sasa!duh hatariiiiiiiiiiiiiii
Kabla ya kufunga ndoa ni vyema ujue uwezo wa mwenzio wa kuvumilia mambo magumu, ufahamu wa jumla, kuchanganua mambo na uwezo wake wa kufanya maamuzi.
baba na mwanawe wote ni mapoyoyo wa kutupwa