Mke wangu ananiletea Usuperstar

Mke wangu ananiletea Usuperstar

Maleven

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2019
Posts
689
Reaction score
3,373
Nilimkuta huyu mwanamke akiwa katika hali duni sana ya kimaisha, sina nia mbaya ya kutangaza shida zake kwakuwa hakuna anaemjua ila nikisema hali ngumu namaanisha ngumu, yaani ile hata ya mlo mmoja shida, kifupi ni ufikara.

Nilipendwezwa na kuwa nibwatu wa kanisani na pia ni kiri kua huyu mwanamke ni mzuri, huenda kwa kipindi kile hakua anajua kua ni mzuri au shida zilimfanya awe humble.

Nilimkuta na baadhi ya changamoto kama maradhi mengine ni y aibu, nimemtibia benga kwa bega bila kumnyanyapaa, mpaka amepona. Kifupi nilijotoa moja kwa moja.

Kosa nililofanya ambalo halikufaa kua kosa ni kumuendeleza kielimu, naona baada ya kutokatoka akaja gundua kua na yeye ni pisi kali miongoni mwa pisi kali.

Nilianza kupata unyumba kwa mbinde sana, mpaka nikaleta uzi humu.

Ila sasa ndugu zangu naona majivuno ya kujiona yeye matawi yanazidi. Ni kama vile mtu anaejiona ana option nyingi sana na kama vile mimi sio level zake.

Kwasasa naangalia watoto tu, niko tayari kwa lolote, mtu mwenye uwelewa mzuri ni baba ake tu, mama ake nao naona pia anampa kichwa mwanae.

Nitakapodhibitisha amenisaliti, tutagawana tulichochuma kiroho safi kabisa, nili muendeleza kwa nia njema, yanayotokea ni maamuzi yake yeye mwenyewe.

Mungu anipe moyo wa kuhimili lolote litakalokuja.
 
Ila kuna watu hawanaga Shukurani huku Dunian hata uwe mwema kwake vipi bado tuu kuthamini wema wa mtu hawawezi,

Pole mkuu ataenda huko yatamshinda

Mungu akubariki kwa kujitolea kwako.
 
Si ulimuendeleza kielimu Ili msaidiane majukumu, basi ndo anakusaidia majukumu hapo
Hapana , lengo ni kua awe na maarifa yanayoendana na dunia ya sasa, aweze kuwalea watoto kwa usahihi, haikua monetary driven desire at all. N hata sasa sijawai muuliza achangie chochote kwenye familia financially, amini mkuu.
 
Kuna namna dunia inakwenda na wengi wenye roho zisizo na msimamo wanapata matokeo kama haya maana hapo kilichokuponza ni huruma pekee na kuona kama atakua mwema siku zote na katika mikasa hii yenye mamumivu naweza thibitisha kuwa mwanaume ni mwaminifu siku zote achana na hizo asilimia 2 za hawa wagaigai
 
Nilimkuta huyu mwanamke akiwa katika hali duni sana ya kimaisha, sina nia mbaya ya kutangaza shida zake kwaku hakuna anaemjua ila nikisema hali ngumu namaanisha ngumu, yani ile hata ya mlo mmoja shida, kifupi ni ufikara...
Usioe mwana mke kwa kimuonea huruma lazima "you will end into tears".....ndoa na huruma its 'a non quid pro quo' issue.
 
Nilimkuta huyu mwanamke akiwa katika hali duni sana ya kimaisha, sina nia mbaya ya kutangaza shida zake kwaku hakuna anaemjua ila nikisema hali ngumu namaanisha ngumu, yani ile hata ya mlo mmoja shida, kifupi ni ufikara...
Kuna siku natembea stockholm Sweden nikapishana na jamaa anaongea kiswahili kwenye simu anang'aka akisema kama anakusumbua kwanini usimfumue tu marinda umkomoe na umpoteezee.

Nilicheka kwa sauti jamaa akageuka kuniangalia naye kuangua kicheko cha hatarii. Sikusimama nikanyoosha with stitches.

The Icebreaker
 
Mungu awasaidie, kuna sehemu amejikwaa akaanguka, apukute vumbi arudi kundini maisha yaendelee.

Wanawake ni viumbe wa ajabu, haijulikani kipi wanataka na kipi hawataki.

Huwa wanapenda amani na furaha mdomoni lakini kiuhalisia ni wepesi wa kukengeuka na kuleta shari ndani ya ndoa pindi amani itawalapo.

Sikushauri uachane, tumia njia zote chanya kunusuru ndoa yako.
 
Back
Top Bottom