Mke wangu anastahili adhabu?

Du sipati picha huyo boss alimkunjaje huyo mkeo,mimi kama mimi kosa la wife kupigwa nao na mtu mwingine, huwa sisamei kabisa hata aje nani hiyo ndio inakuwa imetoka,hiyo ni dharau ya hali ya juu sana.
 
1. Swali unalopaswa kujiuliza ni........... akifukuzwa hapo maisha yakiwa magumu tena, ikitokea kazi inayomtaka afanye mapenzi na boss ndio apate kazi, si atafanya tena?

2. Ukimuangalia kwa uzoefu wako, je unamuona kweli anajutia kosa lake?

3. Kama usingegundua, je ungejuaje?

4. Ni mara ngapi mmekuwa mkiishiwa na anatoa mwili wake ili kunusuru maisha yenu bila wewe kujua?

Akili za kuambiwa, changanya na zako!!!!!
 
Kwahiyo huyo mkeo kaona bora akusaliti wewe na kiapo alichoweka mweli ya Mungu kwa ajili ya kazi? Inaana ikitokea jambo lingine atakuwa tayari kufanya kitu kama hicho kwa ajili ya hela na atakuwa teyari kujiuza kwa ajili ya hela du kaka hapo ana kazi
 
Msamehe na mfanye mpango wa kumtafutia kazi sehemu nyingine.
Haya mambo yapo tuu, utaacha wangapi?. Yeye katoa kwa kuilisha familia (japo siungi mkono), ukimwacha utampata anayetoa kwa burudani tu, tena kwa kuhonga kwa pesa yako!
 
Kimsingi kuna uwezekano Mkubwa sana wife wako akawa still anaendelea na mahusiano na Boss, lakin kwa ninavyo i view situation yako ni kuwa Mkeo alililazimika kufanya hivyo kutokana na hali ya Maisha yenu kuwa Ngumu, the reason as to why hakukwambia ni kuwa yeye alikuwa anaamina, kuwa hiyo issue ataimaliza mwenyewe kimya kimya bila wewe kuja ua, haya mambo yanatokea sana na wala wewe sio wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho, Huu ndo ukweli.
Ushauri wangu ni kama ifuatavyo.
1. Komaa kiume,mfuate Boss wake,mwambie live kuwa asitumie Weakpoint ya Hali ya masiha yenu kuendelea kuwa na uhusiano na wife wako, otherwise utamfungulia mashtaka (Niko tayar kuwa mwanasheria wako).
2. Mpige bit wife, ikiwezekana mstpishe hiyo kazi anayofanya na tafuta other alternative, haimaniishi kuwa Bila hiyo kazi ya wife wako ndo mwisho wa maisha yenu Kaka.
Its better kulala na njaa kuliko kula mafao ya wife wako kumegwa na Boss.

Wasalaam.
 
Du pole sana kwa mkasa huo.mimi nashauri kulingana na bi mkubwa alivyoonesha hiyo honest yake,nadhan ndoa izidi tu kimarishwa kwa faida ya familia
 
yashatokea, asamehe na wasonge mbele, huku mtafute njia nyingine ya kuingiza kipato hapo kwa boss aache tu kazi

Naunga mkono. Kuachana fasta baada ya kosa moja ni rahisi ukiwa nje ya uwanja yaani kinadharia. Maadamu amekiri na anajuta hakuna sababu ya kumwacha.
 
we hujui ufanyaje mpaka sasa? Fanya kile roho yako imeridhia
 

Kuna wakati inabidi ukabiliane na majaribu na kutatua mitihani ya maisha. Kwa kuwa huyo mwanamke amekiri kuwa alifanya hivyo na anajuta kwa yaliyotokea, nashauri umsamehe kwa kosa hilo. Pamoja na msamaha huo ni vema dhambi hii ya uzinzi ikajulikana kwa wafanyakazi wote, bosi aambiwe ukweli na usifanye siri kuficha ficha dhambi hii , kama mkeo hatakubaliana nawe kuweka mambo haradhani ujue bado anapenda mahusiano yao yatendelea, achana naye.

Angalia uwezekano wa kumhamisha mkeo hapo kazini endapo utajiona huna amani akiendelea kufanya hapo. Usisahau kupima afya zenu.
 
mambo ya mapenzi ni mitihani mtupu tafadhali msamehe kama uliwahi kumega vya wenzio.
 
hapo umeliwa fanya maamuzi magumu kama NCCR-MAGEUZI.
 
Mkipata nafasi angalieni picha moja iitwayo A perfect Stranger! Mnawezapata kidogo uelewa wa huyu kiumbe aitwaye Mwanamke ambaye sometimes hufikia hatua hata ya kuzaa na houseboy/shambaboy/mlinzi n.k kwa kisingizio cha kutaka kumsetiri mumewe asiye na uwezo wa kuzalisha!!
 

Amsamehe tu kwa vile amekiri. Bila shaka mkewe ni mstaarab sana na sio mwongo.

Samehe saba mara sabini. Usiwasikilize male chauvenists ambao wao wameshafumaniwa mara kibao na wake zao na wakasamehewa na maisha yakaendelea kuwa na furaha.

Usinunue loneliness.
 

We mama we! Nani kakwambia ulinganishe jinsia mbili ambazo hazifanani? Mwanaume ana nafuu kwa maumbile yake lkn mwanamke hilo ni balaa. Mimi nikimimina mambo yangu kwenye shimo la mtu yanabaki huko huko, lkn wewe ukimiminiwa unayaleta nyumbani na hii ndio sababu unashauriwa kutokumpa kila mtu. Na lini uliwahi kusikia mwanaume amechakazwa na wanawake? Ni wanawake ndio huchakaa maumbile yao kwa kutumiwa na huyu mara yule. Kwanza ni dhalili kwa mwanamke kugeuza mwili wake shimo la taka kuwa kila mwenye uchafu na atupe humo. Na kukudhihirishia mpango huo haupo, nijibu swali langu: ukiingiliwa na wanaume wawili ktk siku yako ya uzazi, huyo mtoto ni wa nani?

Jamani eeh! Si kwamba naunga mkono wanaume wanaosaliti wake zao, ugomvi wangu ni huyu mama salvador kusema kuwa huyu mama kafanya kwa faida. Hakuna faida inayojustify chupi yako kuvuliwa na kila mtu. Siku ukienda DAWASCO wakakuletea usumbufu kukuungia maji, unavua chupi kwa faida. Siku ukienda TANESCO wakazingua, unavua chupi kwa faida. Ukitaka mkopo benki, unavua chupi kwa faida.

Mimi sioni hata cha kushauriana hapo, hiyo ndoa mwisho wake ni hapo. Kaushauri kadogo na kamwisho, kapime ngoma, ujitambue
 
You are right Calinista. Sijasoma hapa hata comment moja inayomhusu mke wa huyo boss ambaye naye pia kazulumiwa, naona kama vile boss ana right ya kufanya mapenzi nje ya ndoa. Mhusika nakuomba Msamehe mkeo muendelee na maisha yenu, kama ambavyo yeye angekusamehe kama angesikia una nyumba ndogo, inawezekana kabisa mama alifanya hivyo kwa ajili ya hali ya maisha and she will have to continue to keep her job. Wadau nanyi msiendelee kumhukumu huyo mama coz non of us is clean na pia dhambi sio uzinzi peke yake. Amri za Mungu ziko kumi uzinzi ni moja tu kati ya hizo na wote tumezivunja tunapaswa kuomba msamaha:embarassed2:.
 
Adhabu unastahili weweusiemfikisha ndio maana kuna makanisa wakiwa wanasomesha mambo ya ndoa wanatoa angalizomsichukue mizigo ilio juu ya uwezo wenu wamechoka kusuluhisha wameona ndoa nyingi watu waakuwa na excess bge wasizoweza kuwabeba ndio maana wamama wanajitokea nje
kazi ipo
 
Ila jamani naomba nisiwatoe povu wadada

Ila kuna kitu is not right with women na kazi zao
Sio shida tu kuna kitu kimeanza jengeka vichwani kwamba bila kuigawa kitu haupati kazi nzuri
Nimekutana na case tofauti lakini ya huyu dada iliniacha mdomo wazi

Ilikuwa conference
Yeye ni afisa serikalini wizara fulani TZ
Siku ya mwisho kuna cocktail part, baada ya kupata kinywaji na aibu kutoka kidogo
Anamfuata binti mwingine Mtz na kumwambia "unaringa nini?"
Wiki nzima umezubaa hapa wakenya wanachukua nafasi zote UN
Uza uc*** upate hela wewe
akaendelea " Mie nimeuza hadi nimepata kazi UN"
Utaishia kuwa maskini
Huyu ni mtu ambaye ana kazi yake na maisha yake nyumbani na isitoshe mke wa mtu

Swali lililonijia kichwani, anahakika gani huyu anayemwambia ana maisha duni huko atokako?
Je ni kweli sasa hivi mwanamke kupata cheo/kazi hadi amegwe?

I was so sad! kwamba wanawake wanaanza kulikubali hili kwa vitendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…