Mke wangu anatapika na kusikia maumivu makali sana

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Wadau nisaidieni,

Mke wangu anaujauzito wa miezi miwili hivi.Anatapika kila mara na anasikia maumivu makali ya mgongo/kiuno.

Nilienda hospital nikakutana na daktari kanambia niuanche tu atulie nyumbani atakuwa sawa, ni ziaidi ya mwezi sasa.

Nifanyeje ili atulie?

Wajuvi wa mambo please.
 
Jibu umeshapewa na wataalamu wa afya kuwa apumzike nyumbani sasa unahitaji nini tena huku JF, la kama unauwezo mpeleke kwa maspecialist wa mambo ya kinamama ila hao mfuko unatakiwa uwe vizui
 
kama mjamzito ni kawaida kama daktari walivyokushauri
 
Hata mimi ilikuaga hivyo hivyo apumzike tu hali itaisha tu kwa wakati wake
 
Jaribu Hosptl ingine
Pia mpatie food supp. kama Spirulina maziwa mbuzi na Mtarangela wa kichina.
 

Mwambie mama avute subira hiyo hali ya kawaida kwa akina mama hasa kma ujauzito ni mara ya kwanza na mimba ni changa hali hiyo inaweza kuchukua miezi miwili hadi mitatu, lkn hali ikiwa mbaya zaidi usisite kumuona Daktari

Tahadhali; usithubutu kumpa dawa yeyote bila ushauri wa daktari
 
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu
 
Hata mimi ilikuaga hivyo hivyo apumzike tu hali itaisha tu kwa wakati wake
Rubii kumbe na wewe ushajifungua? nilikua nakupenda sana, kumbe na wewe umeshafanya tabia mbaya? lahaulaaaah
 
akiamka asubuhi kabla ya kuswaki atafune tangawizi mbichi.
 
Mimba changa zinasumbua hadi unaweza kujichukia loh! Mpe pole ndo ukubwa huo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…