Hii ndo changamoto kubwa ya kumchukua mwanamke kumuoa kipindi ambacho yeye aliona kwako atapata unafuu wa maisha tu pia walau na yeye avae shera.
Sasa ule upendo unaeeendaaa kisha unaanza kupungua, ukishaanza kupungua ndo haya mambo yanaanza kuitana Boss, Mkuu, Kiongozi n.k yaani zile swaga na mahaba hakuna.
Na nnaamini yamkini kuna ishara zingine umeanza kuziona au soon utaanza kuziona.
Usimtukuze, usimbembeleze, usifanye ujinga kumuonesha bado unamhitaji sana na haupo tayari kumpoteza, simana kiume, wewe ni mwanamume.