Mke wangu hajawahi kuniambia ananipenda


Inaelekea hujiamini kabisa wewe pia hujatulia. Je wewe huwa unamweleza kuwa unampenda au unataka akuambie wewe tu? Hebu mwache mtoto wa watu kama ndivyo alivyo. Kakubali kuwaacha wazazi wake na kuambatana na wewe kwa tabu na raha. Hizo chokochoko zako ndo tabu zenyewe anazovumilia. Angekuwa hakupendi angekubali kuishi na wewe mwenye kero za kudai kutamkiwa kupendwa? Acha hizo.
 
Wewe huwa unamwambia kama unampenda! Alaf chagua maneno ya kumwambia mkeo na ya kumwambia girlfriend!
 

Nadhani maneno unayocheua humu na tabia zako vinaendana na ndo mana mkeo huwaa hakwambii kuwa anakupenda! Jirekebishe mitabia yako michafu
 
Uncle action speaks louder than words, acha kero zisizo na mashiko-madhara yake ni makubwa!
 
NAKUPENDA tu ndo linayumbisha ndoa yako hivi kweli uko serious wewe,siamini kama haya uliyoandika umeyafikiria mara mbili.khaaaaaaaaaaaaaa
 
"Actions speak louder than words"....
Je, matendo yake yanaonesha kapoteza upendo kwako, kama si hivyo basi ujue bado wapendeka ndugu
 
Hapo naona mlilazimishana kuoana
 

Nilishawahi kumwambia mmoja humu si kila tatizo lako katika ndoa majibu unapata JF ,na sababu ya yeye kuja JF eti jioni hiyo mke wake anachat sana kwenye simu hamjali...........badala ya kuongea naye kwanza kakimbilia hapa.

Wakati mwingine tunahitaji kukua: Wadada wanataka makalio/chuchu za bandia, wanaume anafikiria kurefusha zakari kibandia,kuongeza urijali kibandia, anataka kutuma sms za bandia kwa patner, ahadi za bandia na mawazo ya utegemezi (bandia)......Mwisho wa siku tunaishi kibandiabandia.

Tuache hayo, by the way Kaunga nakupenda in advance usije kusema tokea nimekufahamu sijawahi kukwambia!
 
Last edited by a moderator:

Kijana inaonekana unapenda kudanganywa au una mapenzi ya Isidingo, kumbuka kuwa binadamu tuko na tabia mbali mbali, mkeo kukupenda si lazima aimbe nyimbo, matendo yake kwako na familia yako ndio yenye usito zaidi. Kwa kweli maneno uliyomuambia si mazuri kabisa,,, nakushauri muombe msamaha na umwambie matendo yake kwako ni muhimu zaidi ya maneno million moja ya kuimba nakupenda!!!
 
kaka heshimu sana huo ushauri uliopewa na akina dada utakusaidia ni lazima kubadilika,the way unavyomtendea ndivyo atakavyo kutendea.Usipende kupoa bali kutoa daima.
 

mtoa mada mie napata hisia zifuatazo:
1. huyo mke umetafutiwa!... siamini kama mlipenda kiasi cha kushibana na kukubali kwa hiyari yenu kwamba mnaweza kuishi kama mke na mume na kujenga familia pengine kwa maisha yenu yote yaliyobaki. na kama mlipendana wenyewe basi zile kauli za awali za nakupenda naamini zinatosha kabisa. Huyo mkeo ni mkomavu wa akili haoni sababu ya kufanya mapenzi ya kinafiki kila ukitoka na kuingia 'i love you' hayo huwa ni mapenzi ya makahaba... chunga sana hizo i love you huwa zimefisha mambo mengi mazito na ya ajabu.
2. wewe mwenyewe hujapevuka akili.. unadhani kuimbiwa I love you kuna maana yoyote katika mapenzi??? mapenzi ni kupendana kwa dhati, kuheshimiana, kujaliana, kuhudumiana, kusaidiana, kushikamana na sio kuambiana kwa mdomo. unapenda bado yale mapenzi ya kitoto.... nakupenda kama azam icecream...! gosh!
3. umeanza kumchoka huyo mkeo... kutokuambiwa I love you isiwe sababu ya kumwambia eti ukipata mwingine atakaekwambia hayo maneno mkeo atajuta... tena una mke mpole sana ingekuwa mie ningekuzaba kibao cha uso!!!
kumwambia maneno hayo mke/mume unaempenda na kumheshimu ni ushamba mkubwa... how could u?
menigne nitarudi baadae......
 
Una umri gani? Maana nafikiri wanaopenda maneno ya aina hiyo hata kama ni ya kejeli ni wale teenagers. Kama umeoa ukiwa na umri wa kutosha, sidhani kama utahitaji kusikia maneno hayo, badala yake utaangalia matendo yake kwako na treatments anazokupa kama mke? Yaani wewe unafikia mahali pa kuweka ndoa rehani kisa unataka kusikia neno nakupenda?

Ngoja nikuulize swali, kati ya hawa utachagua yupi? Una mke mwenye vidume kama vitano hivi kazini na mtaani kwenu, lakini kila siku anakupokea kwa busu na bashasha na maneno mengi ya love. Au una mke ambaye ni mwaminifu, anakujali na anakupenda kwa dhati lakini hana ujuzi huo wa maneno ya bashasha na ya kimapenzi, utamchagua yupi? Mjali mkeo, mpende hiyo alivyo, maneno hayo ya nakupenda na mengine ni just an art, inategemeana alilelewa vipi!
 
Ndoa ya miezi sita tu unaanza kumtolea mkeo maneno makali namna hiyo??kwani toka aache kukwambia anakupenda umepungua kilo ngapi?wewe hua unamwambia??hizi ndoa za kulazimishia hizi zitawatokea puani!
 
hujamfikisha kileleni huyo shemeji yetu. Hapo ndo kila kitu mkuu, wife aliwahi zusha ugomvi ambao hata sikujua umeanzia wapi, ilinikera sana lkn nikasema i have nothing to loose sikutaka kukasirika na najua wanawake wanapenda sana kubembelezwa na kunyenyekewa, nilipotoka job nikasema leo wife naenda kumshangaza. Nilipofika home nikaingia na salaam kuubwa my luuuuuuv upo wapi nikamkuta room, nikampa busu kuubwa akaguna eti sitaki busu la malaya, nikamwambia lzm niwe malaya chumbani kwetu. Bd kanuna hapo nenda kwa hao hao malaya zako, nikamwambia fine niite majina yote leo lkn i just cant stop loving you nikapiga magoti nikamwambia nisamehe kwa kukupenda sana labda unaona kero, akashangaa wewe unanipenda mie, nikamjibu nipe nafasi uone wakati huo nishamkumbatia nimekamata kiuno nikaona pumzi zinapanda, kilichotokea hapo ni kupada mlima kilimanjaro kwa bidii sana wskati yeye anakaribia akasema mume wangu nakupenda sana na wewe unanipenda nikamtaja jina halafu nikamwambia nakupenda sana, lahaulaaa nikaona mtu ananikumbatia wa nguvu zote akimaliza mchezo. Baada ya hapo akaniambia alikwenda saluni flani walipogundua kwamba kaolewa na mngoni wakamwambia umeliwa mmeo lzm ana mipango ya kando kibao ndo yaye akanuna. Sasa ndugu yangu ndani ya ndoa kuwa mwangalifu sana na feelings za mkeo, usipende ku ignore hasa anaponuna, mnuno ni kitu kinasemwa hapo km si mjanja mtaishia kugombana kila siku.usimwonee aibu mkeo mmdadisi kila unapoweza taratibu kimahaba, ukimsifia. Amini usiamini utajenga ukaribu mkubwa sana na mkeo. Ndoa si lelemama ndugu yangu au jaribu kumletea zawadi ya kitu anachokipenda.nawasilisha
 
lakini nikiambiwa hivyo bado najisikia faraja kuliko chochote kile akifanyacho..
 
We nidangaye danganye tuu!!!!!!!!!!ndo unachotaka kufanyiwa wewe....action speak lauder than words..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…