Mke wangu mchafu, nimeongea nimechoka

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
442
Reaction score
1,655
Heri ya X-mass in advance

Ebhana kuishi na mke ambaye hajali mazingira ya usafi wa nyumba ni kero mno. Mwanzo nakutana nae hali hii haikujionesha ila sasa tulipofunga ndoa na kujenga basi hali imekuwa mbaya.

Muda mwingi siishi pamoja na huyu mke kutokana na masuala yake ya kikazi, ila sasa kila anapokuja hapa home asee mazingira yanabadilika nyumba inakua chafu kupindukia.

Akiamka asubuhi anachojua yeye ni kuoga kuvaa na kuendelea na mambo mengine na si kushughulikia usafi wa nyumba nje na ndani. Ana mdogo wake nae ni wale wale, binti mchafu hatari nimeongea sana asee hadi nimechoka.

Hii tabia naona keshamrithisha hadi mwanetu wa kike nae ni ovyo hajui kufagia uwanja, hajui kuosha vyombo nguo zake ni kuziweka popote pale.

Nimeongea sana nimepiga kelele sana ila sioni dalili ya mtu kubadilika. Nikibaki peke yangu hapa home mazingira yanakuwa safi ila akija yeye tu ni balaa kama dampo.

Kwenye maisha yangu nachukia sana uchafu na kukaa na mtu mchafu asiyejali mazingira anayoishi kwa kweli inanipa tabu hadi naona bora niendelee kuishi peke yangu tu.

Mwanamke anajua kuoga, kujiremba kuvaa nguo nzuri ila mazingira anayoishi ni kinyaa kabisa.

Wakuu mnadeal vipi na wake na wanafamilia wengine wachafu wachafu hasa uchafu wa mazingira ya nyumbani nje na ndani?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hilo livumilie tu wengi tunao wana upungufu tofauti tofauti bora huo, wanawake wana udhaifu wa kila aina ila na kuahauri hilo kausha tu una jinsi, huwezi kutoa talaka kisa uchafu,.
 
Cha kufanya ... Amka asubuhi fagia, Osha vyombo.. Deki.. Tandika kitanda.. Fua nguo zao wote.. Zipange vzr.

Fanya hivi kwa muda wa Wiki mbili. Kama ana akili timamu atajirekebisha kama ni chizi ataendelea na hapo ni muda muafaka wa kumpa kadi ya Njano.. Huku ukijipanga kumpa RED CARD.
 
Hilo hamna hana kazi za kufanya eti unamfundisha kazi mtu mzima huyu hapana.
 
Kuishi na mtu mchafu ni ngumu mimi niligombana na ndugu yangu kwa sababu ya uchafu huwa najiuliza Mumewe anaishi nae vipi yaani ni mchafu mno mno.Huyu ndugu yangu nikienda kwake hata maji ya kunywa sitaki unakuta mchafu hadi jikoni ukifungua Freji unaweza utapike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…