Mkenya ashinda taji la malkia wa urembo Afrika

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Shindano la malkia wa urembo duniani la 2017 lilikamilika mjini Sanya China siku ya Jumamosi huku Mkenya Magline Jeruto akishinda taji la malkia wa urembo barani Afrika.

Hatua hiyo inajiri baada ya mwanadada huyo kutoka eneo la Elgeyo Marakwet nchini Kenya kuchukua nafasi ya tano.

Taji la malkia wa urembo duniani lilichukuliwa na mwanadada wa India Manushi Chhillar.

Andrea Meza wa Mexico alichukuwa nafasi ya pili akifuatiwa na Muingereza Stephanie Hill huku naye Aurore Kichenin wa Ufaransa akishinda nafasi ya nne.

Magline Jeruto ambaye ndiye malkia wa urembo wa Elgeyo Marakwet alichukua nafasi ya tano miongoni mwa wagombea 118 katika shindano la malkia mrembo dunia.

Mwanadada mwengine wa Afrika ambaye aliorodheshwa katika nafasi kumi bora ni Ade van Heerden wa Afrika Kusini ambaye alimaliza katika nafasi ya tisa.

Chanzo: BBC Swahili
 
Mkenya ????

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

achunguzwe vizuri asili yake au labda alihamia kenya.
 
_98826849_009c9c03-a9e2-46b9-b9f8-fa3a958fe563.jpg
jMTuSMp1p6ctOWmMagline-Jeruto1.jpg

Shindano la malkia wa urembo duniani la 2017 lilikamilika mjini Sanya China siku ya Jumamosi huku Mkenya Magline Jeruto akishinda taji la malkia wa urembo barani Afrika.

Hatua hiyo inajiri baada ya mwanadada huyo kutoka eneo la Elgeyo Marakwet nchini Kenya kuchukua nafasi ya tano.

Taji la malkia wa urembo duniani lilichukuliwa na mwanadada wa India Manushi Chhillar.

Andrea Meza wa Mexico alichukuwa nafasi ya pili akifuatiwa na Muingereza Stephanie Hill huku naye Aurore Kichenin wa Ufaransa akishinda nafasi ya nne.

Magline Jeruto ambaye ndiye malkia wa urembo wa Elgeyo Marakwet alichukua nafasi ya tano miongoni mwa wagombea 118 katika shindano la malkia mrembo dunia.

Mwanadada mwengine wa Afrika ambaye aliorodheshwa katika nafasi kumi bora ni Ade van Heerden wa Afrika Kusini ambaye alimaliza katika nafasi ya tisa.

Muungwana
 
Na yule mrembo kupitia viti maalumu aliishia 20 "bora", au?!
 
Mbona Mataji yote ya urembo yanaenda Kenya...

Haya mambo mbona kama yana harufu ya ujipu jipu
 
Back
Top Bottom