kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Mkenya atakiwa aukane uraia wa Marekani kabla ya kuwa balozi
Raia wa Kenya ambaye pia ana uraia wa Marekani ametakiwa aukane uraia wa Marekani kabla ya kuchukua nafasi ya balozi wa Kenya nchini Korea Kusini.
Takwa hilo limetolewa na wabunge ambao walikuwa wakijadili orodha mpya ya mabalozi ambao Rais Uhuru Kenyatta amewateua kuiwakilisha nchi hiyo katika nchi mbali mbali duniani.
Bi. Mwende Mwinzi ameteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa Balozi wa Kenya Korea Kusini lakini Kamati ya Ulinzi na Sera za Kigeni katika Bunge la Kenya imekataa kuidhinisha uteuzi huo kwa msingi kuwa ni kinyume cha sheria kwa Mkenya mwenye uraia wa nchi nyingine kuwa mtumishi wa umma. Katika mjadala mkali jana bungeni, wabunge waliunga mkono uamuzi wa kamati hiyo na wamemtaka Mwinzi aukane uraia wa Marekani kabla ya kuchukua nafasi kama balozi la sivyo bunge halitaidhinisha uteuzi wake. Kiongozi wa waliowengi katika bunge Aden Duale amesema hawajamnyima Mwinzi kazi lakini anapaswa kufuata katiba na sheria za nchi.
Bunge la Kenya
Duale amepinga uteuzi wa Mwinzi kwa kuhoji kuwa, je, iwapo Rais wa Marekani atatuma ujumbe wa Twitter na kuwataka raia wote wa nchi hiyo kuondoka Korea Kusini, Bi. Mwinzi atafanya nini?"
Naye mbunge wa Saku Ali Raso alihoji Mwinzi atachukua msimamo upi iwapo kutaibuka mgogoro kati ya Marekani na Korea Kusini. Amesema kuwa na uraia wa Marekani kunaweza kumfanya mwanadiplomasia huyo ahatarishe maslahi ya Kenya.
Kipingee cha 78 (2) cha Katiba ya Kenya kuhusu uraia na uongozi kimetamka bayana kuwa afisa wa serikali hapaswi kuwa na uraia pacha.
parstoday.com