pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
World Half Marathon Championships Gdynia 2020 zilikuwa leo hii kule Poland na mkenya Peres Jepchirchir ameng'aa tena kama kawa. Hii ni baada ya kuweka rekodi mpya(1:05:16 ) na kuvunja rekodi yake mwenyewe kwenye Half Marathon kwa wanawake(1:05:34). Rekodi ambayo aliiweka kwenye Prague Half Marathon wiki sita zilizopita nchini Czech.
Mjerumani Melat Yisak aliibuka wa pili kwenye mbio hizo jijini Gdynia leo hii, huku Mhabeshi Yalemzerf Yehualaw akishika nafasi ya tatu. Wakenya wengine kwenye mbio hizo walikuwa ni Joyciline Jepkosgei, Brillian Jepkorir, Rosemary Wanjiru na Dorcas Kimeli kwenye nafasi za 6, 9, 10 na 11 mtawalia.
Hongera kwake Peres na wenzake pia, kwa kuzidi kuiwakilisha Kenya na kupeperusha [emoji1139][emoji1139][emoji1139] kimataifa.
https://nation.afrika/kenya/sports/...rld-half-marathon-championships-title-2483610