Uchaguzi 2020 Mkihubiri amani msisahau kuhubiri haki ambayo ndiyo Msingi Mkuu wa Amani

Uchaguzi 2020 Mkihubiri amani msisahau kuhubiri haki ambayo ndiyo Msingi Mkuu wa Amani

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
20,419
Reaction score
39,217
Kumekua na kauli nyingi sana hasa kipindi hichi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020 kutoka kwa watu mbalimbali, taasisi za kiraia na kidini, chama na vyombo vya dola pia vikihubiri na kusisitiza amani. Hili ni suala la msingi sana hakuna asiyependa amani.

Ila kumbukeni amani bila haki haiwezi kuwa amani bali ni ukandamizaji na kamwe jamii haiwezi kukubaliana na hili.

Viongozi wa dini, taasisi vyama na Serikali mkihubiri amani msisahau kuhubiri haki ambayo ndiyo Msingi Mkuu wa Amani.

Waachieni raia haki ya kuchagua wawapendao wala msiingilie maamuzi yao. Hapo mtakua mmetenda haki na hakika amani mtaipata bila manung'uniko yoyote.

AMANI NI ZAO LA HAKI
TENDENI HAKI

#MaendeleoHayanaChama
 
Waachieni raia haki ya kuchagua wawapendao wala msiingilie maamuzi yao. Hapo mtakua mmetenda haki na hakika amani mtaipata bila manung'uniko yoyote.
[emoji1534][emoji1534][emoji1548][emoji1548][emoji1536][emoji1536][emoji1536][emoji818][emoji818][emoji818][emoji617][emoji777][emoji777][emoji777]
 
Back
Top Bottom