GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Najua kila Mdau wa Michezo hasa mpira wa Miguu kwa sasa jina la Beki wangu ' mtukutu ' kabisa kwa sasa nchini Tanzania Juma Nyosso halimtoki Kinywani mwake huku wengi wetu wakimshutumu kwamba labda anachangia kuonyesha kwamba mchezo wa Soka / Kandanda ni wa Watu Wahuni na wasiojitambua.
Kwa taarifa yenu tu kama mlikuwa na mawazo hayo mmepotoka na kujidanganya kwani Mimi kama mmoja wa Wadau wakubwa tu wa Mpira wa Miguu na ukizingatia nimeshacheza sana Ligi za Daraja la Nne hadi la Tatu enzi hizo, Shuleni na hadi Vyuoni na sasa ni mmoja wa Waratibu wa Timu yangu tunayopambana ipande Ligi daraja la Kwanza bila aibu wala uwoga nasema ya kwamba wanaoharibu Soka nchi hii ni Waamuzi / Marefarii hasa kwa matendo yao ambayo mengi ni ya Kinyume na Maadili kabisa.
Kwa kuwalindia Heshima hawa Marefa sitowataja majina yao hapa hadharani ila kwa huu Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo Marefarii wanaoongoza kwa kuwatolea maneno ' machafu ' sana Wachezaji ( namaanisha matusi ) hali ambayo huwa inawatoa hao Wachezaji michezo na kujikuta na Wao wanawarudishia kisha wanalimwa / wanaonyesha Kadi Nyekundu na hatimaye kusababisha hizo mechi Kuvunjika na Fujo kubwa kutokea ambazo nyingi huwa zinahatarisha amani.
Mnaoishi Temeke
Nadhani mnamjua yule Refarii mmoja hivi mfupi ana Upara fulani na Utege wa nguvu ambaye Yeye kabla tu hata mpira haujaanza huwa anawaiteni Wachezaji wote mkiwa mmezunguka duara na kuwaambieni....nanukuu na mara nyingi huwa anaanza na lile Tusi letu linalohusu Viungo vya Waliotuzaa kisha utamsikia " Sitaki ujinga katika hii mechi na mchezaji yoyote atakayeleta ukorofi au kidomodomo nampa Kadi Nyekundu hapo hapo na kama akitaka tuzichape / tupigane vile vile nipo tayari ili nimtoe vizuri Bandama akasimulie Kijijini Kwao ". Wakazi wa Temeke na Wadau wa mpira najua mtakuwa tayari mmeshamjua.
Mnaoishi Ilala
Nadhani mnamjua yule Refarii mmoja hivi ambaye huchezesha sana Ndondo zote za Makurumla, Kinesi na mara nyingine hata pale Msimbazi Center zamani Lumumba Rovers ambavyo huwa anafanya kabla na mchezo ukiwa unaendelea. Huyu Refarii mkwara wake tu wa Kwanza pale Timu zikishamaliza tu Kusalimia mashabiki utaona kuna Mtu mmoja anamletea kabisa Panga lake kisha analichomeka katika Shati lake huku Wachezaji wote mkiwa mnamwona halafu akiwaiteni mtasikia akiwaambia maneno haya....namnukuu " Nadhani mmeshaona nimeweka nini mbavuni mwangu sasa Wewe jipendekeze tu Kwangu Mimi nachezesha mpira halafu unanifuatafuata nitakutenganisha hapo hapo Kichwa na Kiwiliwili chako. Ukipigwa Kipepsi au Tama au hata Ndole Wewe vumilia tu na gangamala kwani wote hapa ni Watoto wa Kiume sawa? ". Mnaoishi Ilala nina uhakika mmeshamjua huyu Mwamuzi / Refarii.
Mnaoishi Kinondoni hasa Kawe, Tegeta na ule uwanja wa Mwenge Vinyago jirani na HESLB
Nadhani mnamjua sana huyu Refarii mmoja ambaye Kwanza ni Mstaafu wa Jeshi halafu kibaya zaidi ni Mkurya jinsi ambavyo huwa anawatesa sana Wachezaji hadi kusababisha mechi zake zote anazozichezesha huwa hazimaliziki na kama akizimaliza basi Yeye ile Filimbi yake ya kumaliza mchezo huwa ama anaipigia ndani ya Pikipiki au Bajaji au Gari ya Police ili Kujiokoa.
Ili uone kwamba huyu Refarii kweli hamnazo yaani kabla hata ya mechi kuanza huwa anaangalia ni Timu gani imevaa Jezi ya Njano na Nyekundu sasa ole wenu Timu yenu iwe imevalia Jezi ya Njano siku hiyo mtafungwa hadi mkome kwani anajuikana mno kuwa ni mwana Simba SC wa ' Kindakindaki ' kabisa.
Kituko alichotufanyia hivi majuzi hatuna hamu nacho na nakumbuka Mimi GENTAMYCINE ndiyo nilikuwa na Timu yangu katika mechi yetu na Yeye ndiyo alikuwa Mwamuzi. Kwanza nikiri kabisa kwamba tulimpa hongo / rushwa ili atubebe hivyo katika hali isiyo ya kawaida kabisa kabla ya mchezo kuanza kuna Mchezaji wangu mmoja ambaye kumbe huyu Refarii ana ' bifu ' nae la Kimtaa ambapo ' anambandulia ' Binti yake hivyo bila hata ya aibu akamfuata na kumtukana matusi yote ya Nguoni unayoyajua Wewe na hili kumtoa kabisa mchezoni mchezaji wangu akamwambia maneno haya nayanukuu..." Huna lolote na Kwanza Wewe si umejifanya Kunibandulia Binti yangu sasa Mimi leo nimetoka kulala na Mama yako hivyo kuanzia sasa ujue Mimi ni Baba yako na kwa Kukuonyesha Mimi ni Jeuri Original hii mechi huimalizi ".
Kuona hiyo haitoshi kwakuwa tayari alikuwa kumbe ameshachukua ' mtonyo / pesa ' kutoka Kwetu na baadae tukaja kujua kuwa kumbe hata na kwa wale Wapinzani wetu pia alichukuwa bila ya chembe ya aibu aliwakusanya Wachezaji wote wa Timu zile mbili na kuwaambia mubashara / live kabisa kwamba namnukuu " Oya sikieni nyie Madogo nimeshachukua Pesa kote kote hivyo hapa atakayecheza vyema ndiyo atashinda ila jitahidini muwezavyo lakini Mimi nataka mtoke sare ili msinilaumu ila Timu itakayojilegeza tu itakula Kwake na jitahidini Magoli yenu yawe ya mbali ila ya karibu yote nitayakataa ". Nadhani mnaoishi hayo maeneo mtakuwa mmeshamjua huyo Mwamuzi / Refarii.
Najua wapo Waamuzi wengi sana wenye tabia mbovu, chafu na zisizo za Kimaadili nchini Tanzania ila Mimi GENTAMYCINE nimeanza na hawa Watatu ila na Wewe kama labda uko Dar es Salaam au Mkoani na Wewe pia unaweza Kutiririka na Kuserereka na wako unaowajua na matendo yao yanayohatarisha amani ya mpira wetu ili mwisho wa siku tusije tukawa tu lawama zote tunamtupia Juma Nyosso wakati kumbe kuna akina Nyosso Marefarii wengi tu.
Nawasilisha.