Mkiwasaidia Wasafi TV kwa 'Unafiki' wenu basi upesi sana muwaombe radhi itakayoambatana na 'Fidia' akina Kwanza TV na wengineo mliowafungia nyuma

Mkiwasaidia Wasafi TV kwa 'Unafiki' wenu basi upesi sana muwaombe radhi itakayoambatana na 'Fidia' akina Kwanza TV na wengineo mliowafungia nyuma

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Innocent Lugha Bashungwa ameeleza kuhusu kufungiwa kwa Vyombo vya Habari na Wasanii na kuzungumzia kuhusu Wasafi Tv.

Akiongea katika kipindi cha Clouds Fm Waziri ameeleza haya.

“Kama Wizara jukumu letu la kwanza ni kusimamia nidhamu, inapotokea chombo chochote cha habari au msanii kufungiwa inakuwa wamefikia hatua ambayo hata mimi kama mzazi nimefikia mwisho ndio maana hata lilipotokea la juzi (WasafiTV) tumekaa kujadili tunawasaidia vipi na ninaamini tutawasaidia”

Chanzo: bongofive

Fanya mambo yote mbele yangu ila hakuna Kitu ninachokichukia duniani kama Unafiki na Uonevu hata kama anayefanya ni Rafiki / Ndugu yangu.
 
Nikupe taarifa tu kuwa mambo mengine nchi ya kusadika yanaendeshwa kishikaji tu, kwa kujuana.

Hapo watazuga km mwezi au miezi miwili.

Kwani hujui kuwa kijana alipiga kampeni nchi nzima?
 
ACHA SERIKALI IFANYE KAZI YAKE MKUU HIYO KWANZA TV INA UWEKEZAJI GANI WA KUTISHA?WATU WAMEWEKEZA PALE WASAFI PESA ZA KUTOSHA AFU UWAFUNGIE MIEZI 6 TENA KOSA AMBALO WAO SIO WAHUSIKA WAKUU?
 
ACHA SERIKALI IFANYE KAZI YAKE MKUU HIYO KWANZA TV INA UWEKEZAJI GANI WA KUTISHA?WATU WAMEWEKEZA PALE WASAFI PESA ZA KUTOSHA AFU UWAFUNGIE MIEZI 6 TENA KOSA AMBALO WAO SIO WAHUSIKA WAKUU?
Kwa hiyo KWANZA TV hakuna waliokosa kazi? Hata kama uwekezaji wao ni mdogo kulinganisha na WASAFI?. Sheria ni msumeno.
 
Hivi kumbe kunawatu kabisa walisupport wasafi tv kufungiwa miez 6 kwa kosa kama lile?
 
Nilidhani nilivyopigwa BAN ( kuwa Kolokoroni ) kwa muda mrefu basi nikirejea nitakuta baadhi yenu IQ zenu zimekuwa kuwa bado ni Majuha tupu.
ACHA KUENDESHWA NA MISINGI YA CHUKI HASA KWA WALE AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WAMEKUZIDI
 
Back
Top Bottom