Mkoa gani kuna wafugaji wa ng'ombe wengi, ambapo nitaweza kununua maziwa kwa wingi kuanzia lita 500 nakuendelea?

Kweli aisee , nami nimeona hilo. Nawaza kama kuna lolote linalofanyika kuongeza thamani...
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna wizara nyingine unajiuliza ni za kazi gani....

Mkuu hivi unajua kama Tanzania ni ya 11, kwa uzalishaji wa Nazi duniani na ya kwanza Africa kwa uzalishaji wa Nazi, lakini tunaangiza tani kwa tani za Nazi kutoka Kenya..... Yaaani kuna viongozi wa hii nchi ni mizingo
 
ni kweli mkuu, na kwa wale wanaochunga mifugo ndo wanapata pigo kubwa zaidi
 
Kabla ujamlaumu yoyote je unafanya wajibu wako wa kunywa lita 0.6...au lita 200 kwa mwaka as recommended by WHO????????
 
Tafuta mtaalamu wa mifugo akusaidie kuya identify hayo majani kwenye eneo lako na namna ya kuyatokomeza, pia kama uwezo unaruhusu pandikiza majani lishe (feed)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta mtaalamu wa mifugo akusaidie kuya identify hayo majani kwenye eneo lako na namna ya kuyatokomeza, pia kama uwezo unaruhusu pandikiza majani lishe (feed)

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru kwa ushauri, karibu na shamba langu kuna lile shamba la malisho ya Ngombe la serekali nitapita hapo kuomba mwongozo. Barikiwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hayo majani yapo.

Ni majani fulani yanafanana na mtama... Yaani kwanzia uotaji wake hadi yanapokomaa ni kama mtama na yenyewe yanachanua kama mtama.

Majani haya hudhuru mifugo endapo wakila yakiwa bado hayajakomaa ila yakikomaa hadi stage ya shina lake kupata pingili au kuchanua hayadhuru.

Kinachodhuru yakiwa malaini (hayajakomaa) ni kwamba kati kati ndani kuna maji maji fulan ambayo ndio sumu.

Akila hasa haichukui hata dakik nyingi ng'ombe anajaa gesi tumboni hapo hapo hufa.

Majani haya huota hasa sehemu za mabonde.
 
Steven Nguma na mtama pia vivyo hivyo kama yalivyo hayo majani.

Cha kufanya ni uyafahamu tu hayo majani na mtama kuwa yanadhuru na kuepuka kuwalisha mifugo yako hadi yatakapochanua au kukomaa.

Tiba yake endapo ng'ombe akila ni kuchanganya chumvi kwenye maji na kumnywesha. Unaweza kumpa maziwa pia ila uchanganye na maji kidogo (sio maziwa tupu) na haya yote endapo utagundua mapema na kumuwahi.

Haya yote ni kutokana na uzoefu wangu.
 
Kuna jirani yangu walikufa ngombe 10 kwa kula hayo majani ,waliyafata huko mlandizi
 
Kuhusu maziwa yanapatikana kwa wingi na ubora hapo chawakimu njia ya kwenda kwa sumaye /kisarawe ...kituo Cha kiluvya madukabi Bei 1600 fresh mtindi 1800

Wanayo kwa wingi Sana !
 
Maziwa yapo mengi sana, tembelea Pingo, Mbala, Msoga, Enaboishu, Chalinze nk utapata maziwa ya kutosha, inabidi ufungue kituo cha kupokelea maziwa uwe na tank la kupokelea lenye ujazo walita walao 800 na lina weza kupooza
 
Sio hayo tu yapo aina nyingi sana mkuu majani ambayo ni sumu
 
Njoo Shinyanga maziwa utayakimbia ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…