Mkoa gani unaongoza kwa mbu Tanzania?

Mikoa yetu ni kubwa kujiografia. Zina maeneo yenye tabia ya nchi tofauti. Mbu wanapenda kwenye ardhi oevu na joto kiaina.
Arusha: Mto wa Mbu(Bonde la Ziwa Manyara)
Mbeya: Wilaya ya Kyela karibu yote(Bonde la Ziwa Nyasa), Sehemu kubwa ya Wilaya ya Chunya.
Morogoro: Ifakara na Mikumi
Iringa: Ruaha Mbuyuni.
Kilimanjaro: TPC, Kusini mwa Wilaya ya Same.

Wadau, tunaomba kujua ni Mikoa ipi Inaongoza Kwa Mbu wengi TANZANIA. Mtu wangu wa Karibu AMECHOKA na MBU WA DAR, anataka Kuhama, sasa ili asije ruka Mkojo akakanyaga mavi, hebu changia Mikoa Mitatu hadi Mitano ili aiepuke.

Asanteni wadau.
 
Nilifika Njombe hotelin nauliza net iko wapi wakaniambia kaka tunaomba ukalale huku hakuna mbu,Mbeya Mafinga Makambako hali ni hiyo hiyo hakuna mbu,ila kuna ile baridi ya kutesa haswa.
o
 
Funga kazi ya mbu ni Mwanza Nyashishi,pale kuna mbu kama wanafuga,niliwasha mashine ambayo nasafiri nayo,kwa ajili ya kufukuza mbu bado wakagoma,nikaweka dawa mara tatu wakapungua kidogo.Kesho yake nilihama mwenye ile lodge nikaenda Buhongwa.
 
Hata Butimba mkuu🙌🙌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…