Naoma taarifa umeitafsiri ndivyo sivyo.
Ni asilimia ya umwagiliaji kulinganisha na eneo zima la mkoa husika.
Mathalani, kwa Dar es Salaam yenye ukubwa wa Kilomita za Mraba 1,393. Maana yake asilimia 20 ya eneo lote ndilo la umwagiliaji. Ambapo kwa mantiki husika ni kilomita za Mraba 288.31 pekee.
Wakati Mkoa wa Mbeya wenye kilomita za Mraba 35,954 eneo linalotumika kwa umwagiliaji ni asilimia 16.4. Hivyo eneo hilo ni kilomita za Mraba 5,896.5
Huwezi ukasema Dar inaongoza kwa umwagiliaji kwa kuangalia asilimia ya eneo linalotumika. Kwa sababu Dar ina kaeneo dogo kijiografia kulinganisha na mikoa mingine.
Unachopaswa kuangalia ni ukubwa wa eneo linalotumika.