Mkoa wa Njombe, Mkoa wa Ilala, watu wanabunifu wa njia za kupata ulaji. Langu jicho.
Sasa hivi kuna viwanja vingi sana vya serikali vimepimwa na vinaendelea kutolewa huko KISARAWE na wadau wanavichukua kwa kasi ya ajabu. Taarifa za Uhakika ni kuwa kuna Viwanja vya LOW DENSITY - TZS 1.0 Million; MEDIUM DENSITY - TZS 800,000 na LOW DENSITY - TZS 500,000.
MKuu hii ni habari njema sana,tafadhali unaweza kutumatia maelezo zaidi namna ya kuvipata hivyo viwanja? unajua sio sio lazima tubanane katikati ya mji,kama sisi vijana huko Kisarawe kuna tufaa zana. More details
Mkuu maybe ni Temeke + Kisarawe na makao makuu yawe Kisarawe but not Ilala. Unajua kuwa City Centre ipo Wilaya ya Ilala? Haiwezi kuja akilini kwamba wakazi au wafanyabiashara wa city centre wawe wanawajibika Kisarawe. Hapana
Josm;
Nenda Kisarawe Ofisi ya Ardhi ya Wilaya siku yoyote ya Kazi. Kujaza Form ni TZS 5000 tu. Ukiwa na Pesa ya Kiwanja unalipia hapo hapo na unapewa Kiwanja.
Mkuu Mimi sina uhakika kwani bado ni tetesi. Ila kama ni kweli Kijiografia bado ni sawa. Angalia ramani ni wilaya ya Ilala tu inapakana na Kisarawe:
Mmh haya! tusubiri mkoa wa Bagamoyo naona mikoa ina ota kama uyoga sasa....
sawa Mkuu lakini kama hizi tetesi ni za kweli, naona watakuwa wanachemsha. Yaani Mtu akitoka Kinondoni atakuwa anaingia Mkoa mwingine ndo aende Temeke. Pia kutakuwa na mkorogano mkubwa sana hasa maeneo ya posta, ferry na Ikulu. Katika hali hiyo Ikulu itakuwa Mkoa wa Kisarawe/Ilala na Mkuu wa Mkoa ataishi Kisarawe.
Kama watakuwa wanaamua hivyo, lengo lao ni Dar kuto loose Bandari, Uwanja wa ndege, National stadium na Kigamboni. Otherwise location ya Temeke ndiyo ipo strategic kwa kuungana na Kisarawe.
Mzee mkoa wa bagamoyo tayari,angalia, nyumba za watumishi kajenga magufuli na akaziita za nhc zipo Chalinze njia ya kwenda moro, ni ghorofa,hamna wakaaji na sasa wanakaa popo, bandari ya bagamoyo inajengwa na kupanuliwa (wairan juzi wamesema watasaidia), uwanja mkubwa wa ndege unajengwa bagamoyo(je unakumbuka enzi za KIA na Arusha awamu ya tatu). hizo ndo dalili zenyewe.