Mkoa wa Morogoro na mchezo wa soka.

moudgulf

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Posts
142,674
Reaction score
743,909
Kuna uzi humu unaoelezea kabila furani toka kaskazini ya Tanzania. Mtoa uzi alitaka kujua ushiriki wa watu wa kabila hilo kuhusu mchezo soka. Hilo limenikumbusha mkoa wa Morogoro na mchango wake kwenye mchezo wa soka Tanzania . Morogoro ni mkoa uliobarikiwa kwa kuwa na maji mengi yanayotlilika toka misitu ya milima ya Unguu, Udzungwa na Uluguru. Kutokana na hilo Morogoro inazalisha chakula cha kila aina. Mbali ya hilo mkoa huu umebarikiwa kuzalisha vipaji vya kutosha kwenye muziki na mchezo wa soka. Morogoro ndiyo mkoa wa kwanza Tanzania kuvunja ukiritimba wa mkoa Dar es salaam kwa kujimilikisha ubingwa wa taifa wa mchezo wa soka, pale timu ya MSETO ya mjini Morogoro ilipo chukua Ubingwa wa soka Tanzania kwa Mara ya kwanza nje Dar es salaam mwaka 1975. Leo naomba tuwakumbuke hapa wacheza soka wengi wa mkoa huu, ambao kama siyo wa kwanza kuzalisha vipaji kitaifa basi inaweza kuwa mkoa wa pili nyuma ya Dar es salaam. Naomba Tuwakumbuke wachezaji wafuatao ambao wamekanyaga soka la hali ya juu kabisa Tanzania na ambao wametokea Morogoro ama wana asili ya Morogoro. 1. Gibsoni Sembuli, 2. Mohammed Msomali. 3. Nicodemus Njohole. 4. Deogratias Njohole OCD 5. Boniface Njohole. 6. Peter Tino. 7.Charles Boniface Mkwasa 8. Shiwa. (Mseto) 9. Manga (mseto) 10. Shilingi (mseto). 11. Zamoyoni Mogella "Golden boy" 12. Malota Soma "Ball juggler". 13 Methord Mogella 14.Sahau Kambi "Tanzania one" 15.Mwakingwe 16. Shaabani Kapombe 17. Shiza Kichuya. Karibuni muendelee kujazia wengine na pia tujadili mada hii, ingawa nia si kumbagua mtu kwa kabila lake, mkoa wala kanda. Karibuni
 
1,Aishi Manula
2,Shomari Ali
3,Salum Mbonde
4,Ramadhan Singano
5,Jonas Mkude
6,Hassan Kessy
7,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…