KERO Mkoa wa Shinyanga kuna shida kubwa ya maji

KERO Mkoa wa Shinyanga kuna shida kubwa ya maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Jana nilikuwa na safari ya kwenda Shinyanga kutokea Mwanza. Niliyoyaona njiani wananchi wakiteseka kutafuta maji kweli inasikitisha sana huku tukiwa na Ziwa Victoria kwenye ukanda wa Ziwa.

Serikali ihakikishe maeneo ya Nyasamba, Bubiki, Mipa na maeneo mengi katika Mkoa wa Shinyanga wanapata maji safi na salama.

Pia katika Mkoa wa Mwanza kwenye maeneo ya Runere, Hungumalwa, Mwabuki na maeneo mengi katika Mkoa wa Mwanza Serikali ihakikishe wananchi wanapata maji safi na salama.

Ninamueleza Waziri wa Maji kuwa maeneo mengi katika nchi hii wananchi hawana huduma za maji na zile tambo zake siyo za kweli na hazina mashiko.

Mhe. Waziri chukua hatua za haraka ili tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama linapungua kwa asilimia kubwa.
 
Back
Top Bottom