LGE2024 Mkoani Singida kata ya Utemini, wagombea waliobandikwa ni wa CCM tu

LGE2024 Mkoani Singida kata ya Utemini, wagombea waliobandikwa ni wa CCM tu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mliogwa

Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
37
Reaction score
37
Baada ya majina ya wagombea kutolewa jana na kubandikwa hali ya sintofahamu imeendelea kujitokeza km ilivyo kwenye maeneo mengi nchini.

Mkoani Singida kata ya Utemini ambayo inasimamia mitaa mitatu ya Sabasaba, Utemini na Stesheni wagombea waliobandikwa ni wa CCM tu.

1.Mtaa wa Sabasaba hakuna mgombea wa chama kingine zaid ya CCM katoka nafasi zote

2. Mtaa wa Utemini wagombea wote ni wa CCM isipokuwa mgombea mmoja wa ujumbe ndo anatoka upinzani
3. Mtaa wa Stesheni Majina ya wagombea wa CCM yameandikwa kwa kalamu yenye wino mzito ambayo yanaonekana kwa urahisi tofauti na wagombea wa CHADEMA (ambao wote wanagombea ujumbe.)

Vioja vimetokea katika kata ya Kindai ambapo inasemekana wagombea watatu wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya mtaa HAWAJAWAHI KUCHUKUA FOMU, KUJAZA WALA KUGOMBEA NAFASI YYT ILE LAKINI WAMESHANGAA KUKUTA MAJINA YAO YAPO UBAONI KAMA WAGOMBEA. Wanataka majina yao yatolewe haraka.
Mzee mmoja akahoji sasa kama hapa mjini hali ni hii huko vijijin si ndo kutakuwa na mambo zaidi.
20241109_104544.jpg
20241109_104548.jpg
20241109_104556.jpg
20241109_104600.jpg
20241109_104613.jpg
20241109_104541.jpg
 
Sasa kama uchaguzi wa serikali unaanza kukumbwa na mambo ya hovyo hovyo namna hii kuna maana gani ya kwenda kupanga foleni upige kura wakati tayari wagombea wameshapatikana bila kushindanishwa na wenzao wa upinzani? bora wananchi wasiende kupoteza muda eti kuchagua mtu wa kuleta maendeleo!
 
Back
Top Bottom