tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw Gracian Mukoba amekosoa vikali vitabu vinavyoandikwa na mwandishi wa vitabu na kada wa CCM, Bw Nyambari Nyangwine.
Akiongea kupitia Star TV leo asubuhi ktk kipindi cha 'Tuongee Asubuhi, Bw Mkoba amesema sio tu vitabu vya kada huyo vimeandikwa chini ya kiwango bali pia vinawapotosha wanafunzi. Alitolea mfano wa kitabu kimoja cha Jiografia kinachosema kuwa jua huchomoza kutoka Magharibi na kuzama Mashariki.
Bw Mkoba alishangaa ni kwanini EMAC inapitisha vitabu vya kipuuzi kama hivyo ambavyo vinalenga kuwapotosha wanafunzi huku Serikali ikiwa imekaa kimya bila kuchukua za makusudi kuvifungia vitabu hivyo na kutoa adhabu kali kwa mwandishi husika.
MAONI YANGU
Ndugu zangu nchi hii imeoza tangu juu mpaka chini. Uandishi wa vitabu vya ovyo ni miradi ya mafisadi wakubwa ambao matumbo yao hayajai kamwe. Wanafunzi na walimu kuweni makini na vitabu feki vinavyoandikwa na watu wasioitakia mema nchi hii. Msinunue wala kusoma vitabu feki kama hivyo.
Nawasilisha.
:israel: