Mkoba:Vitabu vya Nyangwine ni feki!

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw Gracian Mukoba amekosoa vikali vitabu vinavyoandikwa na mwandishi wa vitabu na kada wa CCM, Bw Nyambari Nyangwine.

Akiongea kupitia Star TV leo asubuhi ktk kipindi cha 'Tuongee Asubuhi, Bw Mkoba amesema sio tu vitabu vya kada huyo vimeandikwa chini ya kiwango bali pia vinawapotosha wanafunzi. Alitolea mfano wa kitabu kimoja cha Jiografia kinachosema kuwa jua huchomoza kutoka Magharibi na kuzama Mashariki.

Bw Mkoba alishangaa ni kwanini EMAC inapitisha vitabu vya kipuuzi kama hivyo ambavyo vinalenga kuwapotosha wanafunzi huku Serikali ikiwa imekaa kimya bila kuchukua za makusudi kuvifungia vitabu hivyo na kutoa adhabu kali kwa mwandishi husika.

MAONI YANGU
Ndugu zangu nchi hii imeoza tangu juu mpaka chini. Uandishi wa vitabu vya ovyo ni miradi ya mafisadi wakubwa ambao matumbo yao hayajai kamwe. Wanafunzi na walimu kuweni makini na vitabu feki vinavyoandikwa na watu wasioitakia mema nchi hii. Msinunue wala kusoma vitabu feki kama hivyo.

Nawasilisha.
:israel:
 
Huyu Nyangwiene kachangia sana kuharibu elimu nchini! Hili halipingiki!

na bado anazidi kuharibu elimu yetu kwa kuwa vitabu vyake bado vimezagaa mitaani.
 
Huyu Nyangwiene kachangia sana kuharibu elimu nchini! Hili halipingiki!

no thank you. Nataka uthibitisho wa analysis ya kutosha.
Nimewahi kuandika hapa ubovu wa vitabu.

Vitabu vya nyangwine ikiwemo na alivyovifadhili nilivitumia kufaulu.

Nataka aliyevisoma alete ushahidi hapa.

Huo mfano wa mkoba hautoshi kudesqualify kitabu kizima ama kudisqualify vitabu vyote.

HAKUNA VITABU VIBOVU KAMA VYA SERIKALI. Nilitoa ushahidi wa vitabu vya hesabu fm two mpaka fm four syllabus ya 2005. Hapo topic karibu nzima imepotosha. Eg logarithm.
VITABU HVYO NDO VINA NEMBO YA EMAC.

HAKUNA VITABU VIBOVU KAMA LUNDO LA VITABU VYA OXFORD NA VYOTE VINA NEMBO YA EMAC. Na ilipelekea oxford kufungiwa toka mwaka juzi na mpaka sasa hawaruhusiwi kuchapa vitabu.

VITABU VYA nyangwine karibu 96% mpaka sasa havina nembo ya EMAC.
 

mkuu, soma vizuri uzi wangu. nimetoa mfano wa kitabu cha Nyangwine kinachopotosha. Nyangwine kaandika kitabu kinachodai kwamba jua huchomozea magharibi na kuzama mashariki. Aidha, vitabu vyote hasa vya serikali ni vibovu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…