Mapambano Yetu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,130
- 2,102
Mkoloni ulichukua mali zetu na kujitajirisha wewe mwenyewe. Ulijimilikisha mashamba na maeneo makubwa hapa nchini. Ulijenga majengo makubwa na kuwakodisha wazungu huku ukijua wazi kuwa kuna Watanzania wanakufa mahospitalini kwa kukosa kloroqueen wakati huo. Ukaona haitoshi ukafanya kufuru ya kuratibu wizi wa zaidi ya Tsh.150 milioni kwa siku na kwa zaidi ya miaka miwili kwa kisingizio cha nishati ya dharula.
Mmmh! wewe Mkoloni una aibu kweli?
Umeingia mpaka kwenye makampuni ya simu na kuyaamuru yafanye utakavyo. Ukamwendea swahiba wako, na sasa kila anayeposti kinyume na matakwa yako hatarini kushtakiwa.
Mkoloni, nasikia unataka kurudi ili rungu liwe mikononi mwako. Chonde chonde mkoloni, watoto wako umeshawaandalia makazi yao uingereza na kwingineko. Umewawekea kiasi kikubwa cha pesa kwenye account zao mpaka vyombo vya usalama vya kimataifa vimekustukia.Tuache na Tanzania yetu, tuache na umaskini wetu. Yale uliyobahatika kutuibia yanatosha ingawa "mwizi huwa hastaafu".

Hatukutaki wewe Mkoloni urudi kwenu ukachunge Mbuzi.