Ndugu wana JF, Heshima Kwanza.
Baada ya utafiti wa mudu mrefu, imefahamika kua tatiza kubwa la wakulima ambao ndio asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania, wenye kipato cha chini waishio vijijini ni ukosefu wa taarifa za masoko na wanunuzi wa bidhaa zao. Kumekuwepo na juhudi nyingi ikiwamo ya uanzishaji wa vikundi vya wakulima, mfumo wa stakabadhi ghalani, na nyinginezo nyingi lakini bado mkulima wa ngazi ya chini anaevuna gunia kadhaa kwa msimu hajapata ukombozi. Kumkomboa mtu kama huyu ni wazi kwamba unahitaji kumpatia bei halisi ya sokoni na kumuunganisha na wanunuzi moja kwa moja bila kupitia kwa wachuuzi wa kati ambao mara nyingi ndio wanyonyaji wakubwa wa wananchi.
Dhana ua serikali ya KILIMO KWANZA haiwezi kufanikiwa kama huyu mkulima atalima mazao bila kuambia atauza wapi au kumuunganisha moja kwa moja na soko. Kilimo kwanza kitafanikiwa kwa serikali kuwashirikisha wadau binafsi na kuunganisha nguvu ya pamoja kumkomboa huyu mkulima
Kwa kuligundua hilo, Kampuni ya BR Solutions ambayo inafanya kazi ya kuisaidia jamii na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kwa wakati muafaka ili waweze kufanya kufanya maamuzi sahihi, imeanzisha mfumo maalum wa kutumia simu za mkononi ili kuweza kutoa taarifa za bei mbalimbali za mazao katika masoko na kuunganisha wanunuzi wa mazao na wakulima moja kwa moja.
Kupata bei za bidhaa sokoni, mtumiaji wa simu atahitaji kutuma messeji kwa kuanza na neno BEI na kufuatiwa na jina la zao na soko husika, Mfano Bei mcheke kariakoo na kisha tuma kwenda 15450.
kwa mkulima alioko kijijini na kutaka kuuza mazao yake, atatakiwa kutuma messeji akianza na neno UZA MAZAO kisha jina la zao. mfano UZA MAZAO MCHELE MBEYA na kisha tuma kwenda 15450. hapa mkulima ataweza kuunganishwa moja kwa moja na mnunuzi ambaye ameshasajiliwa kwenye mfumo maalum uaotambulika. hii itasaidia kuondokana na wachuuzi wa kati wanaowanyonya sana wakulima.
Kwa wadau wanaofanya biashara ya kilimo sasa ni muda muafaka wa kufanya usajili kwa hiyo kampuni ili kupata taarifa za mazao na kuunganishwa na wakulima moja kwa moja.
Unyonyaji kwa wakulima sasa mwisho.