Hanstz
New Member
- Sep 5, 2022
- 1
- 1
(MKOMBOZI MFILISI) Taifa ili lipate maendeleo watu wake ni lazima wajishughulishe kwenye shughuli za uzalishaji mali ili kuweza kulipa kodi ambayo ndio nyenzo kuu kwa taifa kujipatia kipato ili kuweza kumudu shughuli zake za kila siku na kujenga taifa imara.
Maisha ya Binadamu yana namna mbalimbali za kujikwamua kimaisha na biashara ni moja ya njia iliyoonekana kuleta faida kubwa kwa muda mchache. Binadamu kwa sehemu kubwa ameumbwa na tamaa ya kutamani kufikia sehemu fulani ya kimaendeleo na wengi katika maisha wanatazama hatua za wengine ili kujipa nguvu ya kupiga hatua zao.
Ni jambo lililowazi kuwa sehemu kubwa ya wafanyabiashara Tanzania hawana elimu ya kutosha juu ya biashara zaidi wanatumia uzoefu wa mazingira ya biashara yao na ndio maana wengi wanashindwa kuilithisha biashara kwa watu wengine na inapotokea yule mwenye uzoefu na hiyo biashara amepata matatizo na kushindwa kuisimamia biashara basi hiyo biashara inanafasi kubwa ya kupotea.
Katika hali hiyo ambapo watu wa taifa hawana uelewa juu ya biashara na uangalizi wa fedha lakini sehemu kubwa ya jamii inaumasikini uliotopea sio vijijini wala mijini upatikanaji wa kipato cha siku ni mgumu sana.
Jamii ikiwa imezama kwenye hiyo hali ya umasikini uliotopea, ameibuka mkombozi mfilisi mimi naweza kumuita jinamizi anaitwa mikopo sio siri tena huyu jinamizi kawaingilia wengi na kavuruga kabisa hali ya akili ya sehemu kubwa ya jamii.
Ilitolewa taarifa na TCRA kuhusu usajiri wa laini za simu ni kweli watu wanasajili laini lakini ukifatilia kwa umakini wengi wanalaini zaidi ya moja na sababu kubwa ya kuwa na laini zaidi ya moja ni kukimbia deni kwenye laini ya kwanza naya pili hadi mtu anafikia ukomo wa usajili ni madeni laini zote.
Hapa nchini ilikuja kampuni ya kukopesha ilikuwa inajulikana kwa jina la TALA sasa haifanyi kazi tena Tanzania lakini sababu kubwa ya kukimbia Tanzania ni changamoto ya kulipa madeni hili ni jinamizi ambalo linaangamiza taifa.
Sasa hivi Serikali inatoa mikopo kupitia halmashauri kwa vijana, wanawake na walemavu wakiwa kwenye vikundi kuanzia watu watano. Lakini bado taarifa zinasema ulipaji wa hiyo mikopo ni mgumu sana. kinachorudishwa ni kidogo sana na sababu kubwa wengi wanapochukua huo mkopo wanaenda kugawana na kila mtu anaenda kufanya kile anachopenda kinyume na andiko ambalo liliwapatia huo mkopo.
Sasa ukiingia sokoni watu wanamsongo wa mawazo sababu ya kuwazia rejesho la kila wiki ukienda kwenye familia nyumba hazina amani sababu mke anachukua mkopo kwenye kikundi bila kumpa taarifa mume na vile vile kwa mwanaume, baadae rejesho linakwama ni familia yote inaingia kwenye changamoto na hata familia nyingine zinavunjika.
Ukija mtaani sasa ivi kila kona kuna ofisi za kutoa mikopo yaani jinamizi la mikopo linalazimisha kumkuta kila mtu, mtaa ninaoishi mimi tu kuna ofisi nne za kutoa mikopo hii inajulikana maarufu kama mikopo umiza. Ni kweli inaumiza kweli kweli.
Wakati huo wale wanaopewa mikopo hawana elimu yoyote ya namna ya ukopaji. Matharani mtu anachukua mkopo kwa ajili ya kufanya biashara bila kuangalia kwa undani mazingira ya hiyo biashara sababu tu watu wengi wanafanya biashara hiyo kwenye eneo hilo.
Angalia mikopo inavyowatesa watumishi hasa wale watumishi wa umma. Hali mbaya ya ukopaji inapelekea hata utendaji kazi wa watumishi kushuka hasa kwa upande wa walimu. Mwalimu anachukua mkopo benki huko anakatwa rejesho bado anaenda kuchukua mkopo kwenye ofisi za mikopo mitaani nako anaacha kadi ya banki unategemea huyo mwalimu atakuwa na utulivu gani kuandaa masomo na kufundisha kwa bidii wakati mwisho wa mwezi anaambulia patupu.
Mikopo ambayo ingeonekana kusaidia watu wa taifa lakini sasa inasura ya wazi kabisa ya kuangamiza watu wa taifa. Leo mitandao ya simu ikisema ianze kuwatafuta wale wote wenye madeni yao na kuanza kuwafungulia mashtaka nina uhakika angalau kila familia itakuwa na mtu mahabusu za polisi.
Kuna ulazima kwa upande wa serikali kuangalia upya utaratibu wa ukopeshaji kwa jamii na jamii pia inatakiwa kupewa elimu ya kutosha na pia kughalamia ata matangazo kuamasisha ukopaji uliosalama ili kuokoa jamii. Maana hakuna mtu ambaye atakataa pesa wakopeshaji wao wanajitahidi kutoa ushawishi watu wakope bila kuweka nguvu kwenye elimu juu ya madhara ya ukopaji usio salama.
Upande mwingine usajiri wa ofisi ya kutoa mikopo huku mitaani uangaliwe upwa na zile riba zinazotolewa, kwa sababu kwa hali ya umasikini wa jamii ni ngumu mtu kuanza kuwaza hiyo riba pale anapopewa mkopo lakini linapoanza rejesho ndio uzito wa riba unaonekana na kuleta shida kwenye jamii. Wanaume wengi ambao walikuwa wanajishughulisha na ujasiliamali wamekimbia familia sababu ya mikopo ya hizi ofisi za mitaani.
Nikumbushe machache kwenye misingi ya kukopa usiingie kwenye mkopo kama hauna uhakika wa kurudisha rejesho mfano kuna ahadi ya pesa umepewa ndio unategemea kama rejesho.
Kama unakopa kwaajili ya biashara pesa ya mkopo iwe kwaajili ya kuongezea mtaji na usitumie hiyo pesa ya mkopo wa biashara kwenye shughuli nyingine tofauti na biashara iliyokusudiwa ikapelekea kulipa deni kupitia biashara ambayo ilikuwepo kabla ya mkopo hiyo itapelekea kufilisi biashara.
Jamii inatakiwa kuhamua kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ndio siri ya kufanikiwa kwenye maisha.Watu waache kuchua mikopo yenye riba kubwa kwaajili ya vitu vinavyoweza kusubiria.Matharani mtu anachukua mkopo kwaajili ya kununua sofa au television haya ni matumizi mabaya ya fursa za mikopo.
CHANZO: MWANANCHI DIGITAL
CHANZO MTANDAO

Attachments
Upvote
2