Mkombozi wa kweli kwa Watanzania ni kipi?

Mkombozi wa kweli kwa Watanzania ni kipi?

sindano butu

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2012
Posts
518
Reaction score
181
Habari zenu ya jioni wanajamii forum nimerudi jamii forum kutema cheche zenye tija kwa nchi.

Tumeshuhudia Wagombea mbalimbali wakitia nia kugombea ubunge kwa lengo kuwaletea maendeleo wananchi. Tuache fitina maendeleo ya kweli yanaletwa na wananchi na sio wanasiasa. Hii imejionesha kwenye utawala wa Magufuli ambako kajenga mabarabara kibao, kajenga reli, kanunua madege lakini maisha ya wananchi ni magumu sana mara tano ya utawala ya kikwete.

Sawa nchi imeingia uchumi wa kati lakini imekuja kwa pato la serikali kuongezeka lakini hali za Wananchi ni ngumu sana na mapato ya wananchi kushuka.

Utaletewa lami hadi nyumbani, utaletewa reli hadi nyumbani na mwanasiasa lakini jukumu la kujiondoa kwenye umaskini ni jukumu la Mwananchi mwenyewe kwa asilimia kubwa. Kwa hiyo ukiona watu wanatia nia kugombea ubunge au uraisi ni kwa manufaa binafsi zaidi sababu kuna faida nyingi mno hakuna mwenye nia kukomboa nchi kwa kila mtanzania.

kwa hitimisho ndugu jamii forum tusipende kutegemea mtu fulani ndo anatuletea maendeleo nchini hapana hayo ni mawazo ya kitoto sana na kukubali kuendeshwa kiakili kilakitu na wanasiasa.
 
Back
Top Bottom