Mkongo wa Wolper: Namtaka "LULU" kwa gharama yoyote

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima , inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC ) , Mwami Rajabu ' Mkongo ' ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ' kumalizana' na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ' Lulu' kwa gharama yoyote.

Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si vinginevyo.

"Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper , Husna mara Wema , si kweli , hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi ( Kenya) kwa lengo la kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu, " alisema Mwami bila soni.

Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa ndoto zake. "Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena sana, " alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha zimemtembelea .

Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar , hakuwepo hivyo juhudi za kumpata zinaendelea .
 
wasanii wa bongo wana IQ ndogo sana na njaa ina wasumbua ndio maana kutwa kucha wana jishobokesha kwa kikwete na ccm.
 
wasanii wa bongo wana IQ ndogo sana na njaa ina wasumbua ndio maana kutwa kucha wana jishobokesha kwa kikwete na ccm.

yaani hali mbaya
mtu km lulu nilijua atatulia after the tragedy iliyomtokea
ama kweli tabia ni km ngozi!!
 
Huyo jamaa hana miaka hamsini kweli? maana kama ana watoto sita tena kwa mke wake mmoja lazima atakuwa anamiaka kama 18 ya ulezi,ukitafuta tofauti unakuta kinda la mwanzo kalipata akiwa na miaka 17,na jamaa kama alihudhuria shule ipasavyo itakuwa shughuli pevu! nadhani hiki ni kibabu kilichogoma kuzeeka,hata aproach zake za kizeezee!
 

Dunia hii imejaa majuha sana aiseeee! Jitu zima na ndoa ya watoto sita lakini linatamka hayo maneno!!!! Mbuzi tu huyu, Wala hana ishu.
 

Kuna watu majuha sana Mkuu!!!! Ati linamtaka Lulu kwa garama yoyote, aanze na watoto wake hao sita!!!!
 
Kuna watu majuha sana Mkuu!!!! Ati linamtaka Lulu kwa garama yoyote, aanze na watoto wake hao sita!!!!

Linatafuta umaarufu mbwa hili, halafu mke wake nae anasikiliza upuuzi wa mumewe, mmh kwa hali hii acheni tu jide na gadner waachane
 
Wakongo walivyooo, warumi hebu weka pichaaa
 
Hivi akili za akina domo unaweza zifanyia nini?

Zile hutumika kuvutia wapuuzi na watu duni wenzao....

vipi si hata bi harusi Juliana Shonza mmemfanyia hivyo mpaka mwigulu kalamba kisha mmemtupia msukuma wa watu makombo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…