Mkono wa kushoto ni dharau, nimfanyaje au nijilinde vipi?

Mkono wa kushoto ni dharau, nimfanyaje au nijilinde vipi?

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Habari wanazengo, mimi nina duku duku kidogo kuhusu watu wanopenda kutumia mkono wa kushoto ili hali siyo watu wa mikono ya kushoto.

Kuna mwana mmoja mtaani hapa ninapokaa yeye mara nyingi ukikutanana nae mkisakimiana nae yeye huwa analeta mkono wa kushoto na siyo mara moja au mbili like all the times. Siyo tu katika kusalimiana tu hadi kitu kukupa au kuchukua anchukua kwa mkono wa kushoto.

Mimi assumptions zangu inaweza kuwa mwana ana kaimani kakishirikina haiwezekani utumie mkono wa kushoto.Kuna siku jamaa wengine walimshiktukia(hawa wanaonekana ni wajanja) alivyotaka kuwa salimia nao wakatoa wa kushoto.

Hii ina maana gani? au nijilinde vipi kama ni mambo ya kishirikina?
 
Habari wanazengo, mimi nina duku duku kidogo kuhusu watu wanopenda kutumia mkono wa kushoto ili hali siyo watu wa mikono ya kushoto,
Kuna mwana mmoja mtaani hapa ninapokaa yeye mara nyingi ukikutanana nae mkisakimiana nae yeye huwa analeta
Puuzia au mpe na wewe wa kushoto!
 
Ni kweli Nyerere aliwahi kuvaa gloves kusalimiana na malkia?

Dawa ya mabishoo ni kuwa Bishop zaidi yao - Sugu
 
Watakuja kukuuliza uo mkono wa kushoto anakufanyia wewe tu, au wote?
 
Lakini kuna watu wao tangu kuzaliwa wanatumia mkono wakushoto, nakumbuka tukiwa shuleni tulikuwa tunasoma na watu wa aina hii , wanotumia mkono wa kushoto kuandikia , tulikuwa tunawaita MASHOTO!

Sio kuandikia tu, wengine hata kutanyia shughuli zao za kila siku, wamezoea kutumia mkono wa kushoto, ukimwambia atumie wa kulia hawezi kabisa!

Wengine hata miguu , hutumia mguu wa kushoto kucheza mpira nk... Tunao wachezaji wengi Sana wanaotumia mguu wakushoto, vipi na hawa nao wana Imani za kishirikina?!

Sidhani kama kila mtu anayetumia mkono au mguu wa kushoto Basi ana element ya imani za kishirikina! Tatizo linaweza kuwa kwenye tafsiri yetu sisi wapokeaji wa mambo!

Mashoto wengi huzaliwa hivyo, wengine ni malezi na makuzi tangu utotoni, sio vizuri kuwahukumu katika hili.
 
Miki natumia mikono yote miwili bila.shida kabisa.
Na wenye nguvu ni wa kushoto though kuandika naandikia kulia.
Kula nalia kushoto, ugali nafinyia kulia.
Na vitu vingine kibao.
Inategemeana tunakuatana vipi, naweza kukupa huduma au kupokea kwa mikono yote miwili na wala nsione soo .
It doeant mean mimi n.mchawi.
Mostly haya mambo n imani yako tu, bit if u dnt believe in this shit u good to go.
 
Heb tuwe great thinker kidogo..nikitoa mkono wangu wa kushoto na wewe wa kulia ina match vp? Iweke kwenye uhalisia
 
kwan mkono wa kushoto una shida gan? kamaa una nuksi ukate wako ulishe mbwa african type...
 
Habari wanazengo, mimi nina duku duku kidogo kuhusu watu wanopenda kutumia mkono wa kushoto ili hali siyo watu wa mikono ya kushoto.

Kuna mwana mmoja mtaani hapa ninapokaa yeye mara nyingi ukikutanana nae mkisakimiana nae yeye huwa analeta mkono wa kushoto na siyo mara moja au mbili like all the times. Siyo tu katika kusalimiana tu hadi kitu kukupa au kuchukua anchukua kwa mkono wa kushoto.

Mimi assumptions zangu inaweza kuwa mwana ana kaimani kakishirikina haiwezekani utumie mkono wa kushoto.Kuna siku jamaa wengine walimshiktukia(hawa wanaonekana ni wajanja) alivyotaka kuwa salimia nao wakatoa wa kushoto.

Hii ina maana gani? au nijilinde vipi kama ni mambo ya kishirikina?
Mkono wa kushoto hauna tatizo lolote lile.

Tuache imani mbaya.
 
Back
Top Bottom