Tujasaidiane wadau, najua huo ni mkono wa kulia lakini kwanini uitwe ni mkono wa kuume? Je, hili nalo ni sehemu ya mwendelezo wa kuwanyanyapaa wamama? Kinyume cha mkono wa kuume ni ipi? Kwangu hili naona utata. Karibu tupanuane mawazo.
Nashukuru nimeona ingawa haijadadavuliwa vilivyo! Nilichokiona zaidi ni kuwa kiswahili ni chetu kinatutesa na wala hatuonekani kukijali, ivi lugha zingine zitafanyaje? Najifunza kichina, kama lugha yangu inanipa shida; nitafanikiwa kweli?