Hiyo 21% ni interest kwa mwaka na kwa kuwa utakaa na hela zao kwa miaka 4 hiyo interest ingekuwa 21%x4= 84%, lakini kwa vile utakuwa unalipa kila mwaka hiyo rate ya 21% itakuwa inapungua kila mwaka kutegemea na ulivyolipa lakini commulative itakuwa inaongezeka at a decreasing rate (yaani inaongezeka kwa kupungua) ndiyo maana after 4 years hautakuwa umelipa 84% lakini uki calculate utakuta interest rate ni zaidi ya mara mbili ya ile waliokuandikia kwenye makaratasi, hiyo ndiyo inaitwa effective interest rate.
Ukitaka kujua effective interest rate unayolipa wewe chukua tu total interest amount gawanya kwa loan amount, lakini kumbuka the higher the repayment period, the higher the effective interest rate and hence higher interest amount. Mfano kama mkopo wako in wa mwaka mmoja utalipa interest hiyo hiyo waliyokuandikia kwenye makaratasi yao, hali inakuwa mbaya pale unapotaka kulipa kwa muda mrefu ambayo ndiyo benki wanapenda kwa kuwa watapata interest kubwa.
Ushauri: Jitahidi kuchukua short term loan kuliko long term loan.