Inahuzunisha sana, msomi kama wewe ambaye umesoma mpaka PGD huelewi jinsi mkopo unavyotolewa.
Kimsingi, taasisi za kibenki zinatoa mkopo kwa kuweka rehani kitu chenye thamani sawa na mkopo uliouchukua. Yaani, kama unataka mkopo wa 20m uhakikishe kuwa una mali (ardhi, nyumba) yenye thamani zaidi ya 20m. Hii ni ili endapo utashindwa kurudisha fedha zao basi wauze hicho kitu na hela yao irejee kwenye system.
Vyeti vyako sawa, vinaweza kuwa vimetumia fedha nyingi na akili pamoja na muda kupatikana. Lakini taasisi husika haiwezi kuviuza baadae na kurudisha hela yao. Potelea mbali, uuzwaji wa cheti ni marufuku na hauruhusiwi kisheria.
Na baadhi ya taasisi tu zinazotoa mkopo mdpgo sana bila kuweka kitu rehani. Na mara nyingi haizidi 500,000. Namaanisha M-PAWA , L-MICROFINANCE na nyinginezo. Hao watakufatilia wanavyojua wao. Benki hazina huo utaratibu. Hata kama umesomea Harvard, hawataki vyeti vyako.
Pole sana Mkuu ila usikate tamaa. Mungu atakuwezesha.