SoC02 Mkopo si sababu kuu ya Vijana wengi kushindwa kujiajiri au kuanza biashara zijue sababu nyingine?

Stories of Change - 2022 Competition

Sylvesterjohn

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
4
Reaction score
3
MKOPO SI SABABU KUU YA VIJANA WENGI KUSHINDWA KUJIAJIRI AU KUANZA BIASHARA ZIJUE SABABU NYINGINE?

Changamoto ya ajira kwa vijana ni suala lisilo kosekana katika jamii zetu hasa kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali na vijana wadogo ambao walishindwa kuendelea na masomo.Kati ya vijana kumi ,vijana saba pekee hueleza kua sababu kubwa wao kushindwa kujiajiri ni uhaba au kutokuwepo kwa mkopo au kiwezeshi ili kuanza biashara zao au kuendeleza .

Hakika mkopo hauwezi kua sababu ya vijana kushindwa kujiajiri jambo hili nimelifanyia ufumbuzi kwa vijana wengi hasa wahitimu na pia walioko mtaani bila kufanya chochote hivo kuja na sababu ambazo vijana hushindwa kujiajiri na kuachana na sababu ya kukosa mkopo mbali na kwamba taasisi binafsi na serikali zimekua zikitoa mikopo kwa vijana wengi sana.

ZIFUATAZO NI SABUBU ZA VIJANA KUSHINDWA KUJIAJIRI AU KUANZA NA KUENDELEZA BIASHARA ZAO MBALI NA MKOPO…

1. UWEPO WA MAWAZO(MATAMANIO) MENGI KWA WAKATI MMOJA.
Siku zote matamanio ni jambo ambalo huweza mtoa mtu katika jambo(muhimu) hasa pale anapoa kuwa na idadi nyingi ya mawazo(matamanio).Jambo hili linatokea sana kwa vijana wa kitanzania maana huwa na mawazo mengi ya kufanya ili kufikia mafanikio yao jambo hilo huwafanya kutokua na maamuzi sahihi hivo hatma yake kuangukia kwenye chagua la biashara ambayo haiwezi kumfanikisha au kuleta matunda .Hii ni kwa upande wa kwanza wa vijana wenye mawazo lakini hukosa chaguo sahii.Kitaalamu hii huitwa “DIlema”kama msemo usemao mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote.

2.KUKOSA SUBIRA AMA UVUMILIVU.
Mafanikio ni mkusanyiko wa matukio au jambo ambalo hufanyika kila mara kwa juhudi bila kukata tamaa ,hii ni maana inayosadikika kusemwa na matajiri wengi kama ushuhuda kwao.Vijana wengi wamekua wakikosa Subira ama uvumilimu kwa jambo wanalofanya kutokana na kuchelewa kwa matunda ya jambo hilo kama tulovotarajia ,hivo kupelekea kuacha au kukata tamaa kufanya hilo jambo.Tafsiri hii ni tofauti kabisa hasa pale mtu unapoamua kuanza biashara maana matunda yake huweza chukua mda mrefu kujionesha hivyo kuenda kinyume na vijana wa sasa ambao hutaka mafanikio kwa haraka.Kiufupi mi kwamba hakuna biashara yenye matunda kwa mda mfupi katika hii dunia na wengi wanaotaka hivo huishia kutapeliwa na kupoteza fedha nyingi sana katika Maisha yao.

3.KUKOSA UTHUBUTU.
Kutokana na mitaala yetu ya elimu ambayo imejikita Zaidi kufanya jambo kwa usahihi bila kukosea ,imeathiri vijana wengi sana katika kuwa na uthubutu wa kufanya biashara Fulani akihofia kushindwa,huku maswali mengi yakiwa ni
  • Changamoto ya biashara hiyo?
  • Hofu kupoteza fedha?
  • Hasara za biashara hiyo?
Jambo hili huwatokea hasa wahitimu na vijana wengi wenye elimu ya nyanj’a mbalimbali ;ndo maana wengi wanaodumu katika biashara ni wale ambao hawana elimu au wana kiwango kidogo sana cha elimu (darasa la saba)kwa maana wao hujikita katika biashara bila kujali hasara zake.

4. KUSUBIRI MAHITAJI YOTE YA BIASHARA KUJA KWA WAKATI MMOJA.
Katika kuanza biashara ni jambo ambalo haliwezekani kupata vitendea kazi vyote kwa wakati mmoja.Hii imekua kinyume na vijana wa sasa hasa wanapoanza biashara hutaka kupata kila kitu ndo waanze shughuli yenyewe kabisa .Hatua ni jambo la msingi katika kila jambo hapa duniani ndo maana hata katika familia mtoto huanza kwa kukaa,kusimama hadi kutembea na mambo mengine ,hivyo katika biashara mwazoni vitu vya msingi ndio huhitajika na vingine hufatia.Mfano unataka kuanza biashara ya kuuza matunda huwezi anza kuuza kila matunda bali utaanza na yale ambaya yapo ndani ya uwezo wako na baadaye kuongeza matunda mengine ,badala ya kusubiri kupata matunda yote kwa wakati mmoja na mwishowe kushindwa kabisa kuanza biashara hiyo.

5.KUKOSA MAARIFA SAHIHI.
Vijana wengi hukosa maarifa sahihi hivo kupelekea wao kukata tamaa katika biashara wanazotaka kufanya. Hakiki uwepo wa maarifa sahihi humwondoa mtu kukata tamaa, kutokana na Imani ambayo amejijengea katika hayo maarifa. Kiufupi maarifa sahihi hupatikana katika usomaji wa vitabu vya kimaendeleo jambo ambalo ni chamgamoto kwa vijana kusoma vitabu .Hii inafanya nieleze kisa cha kijana mmoja ambaye Baba yake alikua ni mwenye mali sana lakini alikumbwa na maradhi sana ambayo yalifanya muda wote awe hospitalini kuuguzwa,na siku zilipokalibia za yeye kuuguzwa kutokana na taarifa ya wauguzi .

Baba huyo alisema maneno haya kwa mwanae kabla ya mauti akimpa kitu mkononi “mwanangu urithi wangu kwako ni kitabu ambacho kimenifanya nipate utajiri huu hivo mwanangu nakusihi ukisome ili uweze kuendeleza utajiri huu kwa ukoo wetu” kijana alishangaa sana maana alidhani Baba yake atampa mirathi ya kampuni zake na hati miliki ,hivyo akapuuzia na kutokana na yeye hakua maskini kivile akachukua kile kitabu na kuhifadhi katika maktaba ya nyumba yake na baada ya mazishi Maisha yaliendelea .Miaka kadhaa mtoto wa yule kijana ambaye ni mjukuu ya yule mzee aliyefariki aliingia maktaba na kuangalia kile kitabu alichokiona alistaajabu sana. Kitabu kile kilisheheni idadi ya kampuni ambazo alikua nazo yule mzee Nje za nchi na benki ambapo mapato yalihifadhiwa pamoja namba ya siri ya hiyo benki.Nadhani kuna jambo la kujifunza hapo.kama yule kijana angekua mtu wa kutafta maarifa kupitia vitabu basi angesanukia huu mchongo mapema kabisa.

HITIMISHO
Mkopo ni moja ya kitu muhimu unapaonza kufanya biashara ila ni muhimu kujua vitu vingine Zaidi maana fedha pekee sio muhimili wa kuweza kufanya au kuendeleza biashara yako.

Ndugu kijana; hakikisha biashara yako ina mikakati mathubuti na yenye tija ,pamoja na changamoto ambazo utaweza kuzitatua pasipo kukata tamaa. Jitahidi pia kuwa mkweli katika shughuli yako na mwaminifu lakini pia uwe sehemu ya biashara yako.

AHSANTE.
 
Upvote 2

Naona Kama umegusa point bingwa unastahili kura yangu,umeongea vitu vilivyondani hasa ya tatizo la vijana kushindwa kujiajiri/ujasiria mali
Thanks🙏🙏
 
Back
Top Bottom