Mkopo unaitajika: Je, naweza kupata mkopo usio na riba?

Mkopo unaitajika: Je, naweza kupata mkopo usio na riba?

Msumb

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2022
Posts
3,452
Reaction score
5,372
Mambo vipi wana jukwaa mko poa, wazima nyote, nije kwenye shida yangu hii, nauliza naweza kupata mkopo wa kama sh laki moja bila riba, au kama riba ipo iwe nafuu kidogo,

Kuna shida naitaji kuzitatua kidogo kama kuna uwezekano nikapata mkopo, kuhusu uaminifu ndo nguzo kuu, je naweza kupata mkopo ndugu zangu itawezekana 🙏
 
Hapo hapo ulipo kuna jirani yako anaweza kukupa. Mfate

Pia kwenye contacts zilizopo kwenye simu yako kuna mtu anayo. Wapigie simu unaofahamiana nao uwaombe wakukopeshe
Mkuu mawazo yako ni mazuri ila hayapo sahihi
 
Unaweka nini kama bond mzee? Inakaa siku ngapi?
Sijajua niweke nini bond kiongozi, pia kuhusu kurejesha naomba niwe narejesha kila jumatano boss sh elfu nne nne kama hutojali ndo uwezo wangu
 
Kagalegale kwa ndugu na jamaa zako wakupe hiyo 100,000
Hii mbinu tuliwahi kufundishwa kwenye Entrepreneurship kama njia moja wapo ya kupata Mtaji unapotaka kufanya biashara/Ujasiriamali.

Ila nimegundua njia hii haiko Practical sana huku Afrika especially Tanzania.

Watanzania wengi tuna roho za Kukunja, tunapenda kupigiwa magoti kila siku kuombwa mia mbili mbili badala ya kutaka kuwezeshana.
 
Naweza kuweka vyeti vyangu na kadi ya nida au kitamburisho cha kupiga kiongozi
Kama hadi unaweka Cheti seems utakuwa ni muhitaji sana.

Kama hautajali unaweza kusema walau kiufupi lengo la hiyo laki 1 unayoomba.

Kama unataka kuifanya mtaji au unakwenda kusolve shida yako tu privately. Ingefaa iwe mtaji manake unasema unaweza kurejesha elfu 4 nne kila wiki
 
Kutatua shida zangu private, pia kufanya mtaji pia mkuu yani vyote kwa pamoja pia mkuu
 
Kutatua shida zangu private, pia kufanya mtaji pia mkuu yani vyote kwa pamoja pia mkuu
Siku hizi ishu za utapeli zimekuwa nyingi kidogo kwahiyo watu wamepoteza imani.

Wengine tuko mbali hata hiyo dhamana ya Vyeti itakuwa ngumu kutufikia.

Unaweza kufanya utaratibu uweke bond/uuze hiyo simu janja yako ambapo hautakosa laki 130,000 hadi 200,000 kutegemeana na aina ya simu uliyonayo then utapata hiyo laki 1 yako na fedha ya kununua simu ndogo ya 25,000 hadi 40,000.
 
Sawa bana mkuu
 
Mtoa mada unazingua yani mtu akukopeshe bila riba halafu marejesho ni 4000 kwa wiki? Deni litaisha baada ya wiki 25 almost ni miezi 6.Mkopo huo haupo.
 
Mtoa mada unazingua yani mtu akukopeshe bila riba halafu marejesho ni 4000 kwa wiki? Deni litaisha baada ya wiki 25 almost ni miezi 6.Mkopo huo haupo.
Uwezo wangu hapo ndo ulipoishia siwezi kuforce kitu wakati sina uwezo nacho nimeongea hali yangu halisi, ndo maana kuna kuwezekana na kushindikana
 
Uwezo wangu hapo ndo ulipoishia siwezi kuforce kitu wakati sina uwezo nacho nimeongea hali yangu halisi, ndo maana kuna kuwezekana na kushindikana
Huna ndugu? Majirani hapo unapo ishi hawapo? Au marafiki, badala ya kuja mitandaoni..huko ndo utaaminika kwa hyo riba
 
Back
Top Bottom