Mkopo wa biashara

babu kwani huwa unavuta? Halafu kulikuwa na thread humu jamaa wana ofisi yao wanakopesha. Jaribu kuisearch babu. Unataka mkopo wa benki au hata hizi asasi zingine za fedha?

Hapana Hus,

Babu hajawahi kuvuta bangi wala petrol, ila anaamini kawa waswahili wenzake kwamba kila mtu ana degreee fulani ya kichaa!!

Iwe bank au la, babu hana neno ili mradi siyo wababaishaji!!

Babu DC!!
 

Kama unawajua wewe leta details,

Ulitaka niweke na credit history zangu hapa??

Kama umefuatilia mjadala basi utakuwa umegundua kuwa mie si mbumbumbu wa mikopo.

Babu DC!!
 
nimepata akili sasa,
ngoja nihamishie tangazo langu humu kumbe ndo kwenye wasomi.
 
Mzee DC, ushauri wangu mkubwa pamoja na yote vilevile utembelee kwenye hizo bank mwenyewe ili uweze kupata information zaidi kabla hujaamua kwenda na bank gani kwa mkopo.
 
Kwa uhakika katika biashara yeyote pesa haichukui naafasi ya kwanza. Kuna mapesa mengi yamelala nchi hii kwa kukosa watu wenye vitu vya kufanya. Yeyote mwenye kitu cha kufanya, {wazo zuri la biashara} atapata tu pesa za kutosha. Usitabute pesa shs 100 milioni au 1billioni bila kuwa na andiko la mradi. Siyo wewe unayejua utataka kukopa shs ngapi. Mchanganuo wa biashara yako ndio utakaokuambia unatakiwa uikopee biashara yako kiasi gani.

Wasiliana nami nikupe mawazo ya biashara, uandikiwe mchanganuo, nikuoneshe wakopeshani, nikupe biashara ikibidi na hata dhamana nitakutafutia kwa masharti nafuu. Usijali kuhusi interest rates, jali aina ya biashara unayotaka kuifanya. Kuna biashara ambazo unaweza mudu interest 48% kwa mwaka kulingana na gharama za uendeshaji.
 

mkuu nimeku-PM
 
May be niongeze dimension nyingine,

Kama naagiza bidhaa nje..na tayari nina LPO ya customer kuonesha kuwa huo mzigo tayari utauzika kwa customer ambaye tayari yuko tayari kutoa uthibitisho.

Watu gani wanatoa mikopo katika case kama hii??

Babu DC!!
ujue babu dc ubaya wa benk zetu ni collateral based na sio cash flow based.hawajui kwamba mtu unaweza kuwa na collateral ukachukua mkopo na ukashindwa kulipa
nadhani hii ni challenge kwa benki zetu wawe wanaangalia cash flow na return yake na sio macolateral yasiyokuwa na maana ndo maana defaulters wanakuwa wengi
 

Ahsante sana ndugu yangu,


Sitapenda kuichukulia negative comment yako ila ina mwelekeo kama ule wa Mkuu mmoja aliyesema kuwa Watanzania ni wavivu wa kufikiria...Na mwingine akasema mara nyingi tunakuwa na wivu wa kike....!!

Ninaposema kuwa natafuta Bank au taasisi ya pesa inayokopesha 100mil to 1biln, nina maana kwamba tayari ninayo biashara ambayo naona capital ninayohitaji iko kwenye hiyo range..Na pia naaamini kuwa kama nikipata mkopeshaji mwenye masharti rafiki (friendly terms) naweza kurudisha mkopo wake bila matatizo ....assuming hakuna unforeseen events!

Kwa hiyo mambo ya andishi sioni kama ni muhimu endapo sijui naenda kukopa wapi. After all, maandishi feki yapo kibao na watu wanachukulia mikopo kila siku ila mwishowe wanashindwa kulipa.

I wished tungeongea ki-practical zaidi badala ya kuwa too theoretical!!
 

Ahsante sana Smile,

Hili ndilo tatizo langu kubwa...

Nina friend kutoka Kenya ambaye anasema kuwa wenyewe wako mbali sana...Kwamba kama meshafanya kazi na benk kwa muda kidogo, inafika mahali wanakupa mkopo (within limited range, kama 5mil Ksh, about Tshs 90mil) bila dhamana yoyote. Leo nimetoka CRDB wakanambia kuwa hata 2mil, lazima niwape hati ya nyumba!!

Sijui kwa nini bank zetu zinakuwa hivi...Au wanaamini kuwa hizo pesa wanatakiwa kuziatamia ili baadaye zitotoe vifaranga!!

Babu DC!
 
Nimeku PM mkuu
 
Mzee DC, ushauri wangu mkubwa pamoja na yote vilevile utembelee kwenye hizo bank mwenyewe ili uweze kupata information zaidi kabla hujaamua kwenda na bank gani kwa mkopo.


Ahsante sana BJ,

Nimejitahidi kutembelea baadhi ya banks ili nilidhani kwamba hapa kuna wataalamu wa mambo ya fedha ambao wangeniongezea taarifa hizi muhimu. Halafu taasisi zinazotoa mikopo ni nyingi sana, kiasi kwamba ni vigumu kuzifikia zote!

Kwa hiyo wenye taarifa wakituwekea hapa itasaidia sana!

Babu DC
 

Kibananhukhu

are you there?
 
May be niongeze dimension nyingine,

Kama naagiza bidhaa nje..na tayari nina LPO ya customer kuonesha kuwa huo mzigo tayari utauzika kwa customer ambaye tayari yuko tayari kutoa uthibitisho.

Watu gani wanatoa mikopo katika case kama hii??

Babu DC!!

Kuna jamaa yangu alikuwa na case kama hiyo, benki nyingi hawakukubali, hatimaye alipata benki moja hapo mnazi mmoja kama unatoka mnara wa saa, kushoto kabla ya mataa m.mmoja.


Yupo jamaa yangu mwingine, amepata CRDB lakini wanampa kwa mafungu say anahitaji mil 900, wanampa m 200 au 300. Kikwazo wanachosema wao, hana historia ya kurudisha mkopo mkubwa. Historia unapata wapi? Ndiyo yale yale, tunataka uzoefu wa kazi miaka 5, unapataje uzoefu, fanya kazi ndogondogo ili ufike pale unapotaka.
 

Ahsante sana ndugu yangu,

Hiyo bank iliyoko Mnazi mmoja inaitwaje? Ni Dar Community bank au??

Hayo maelezo mengine ni muhimu ila huweza kujipanga kama hata hujui nani anaweza kukupa mkopoa!!


Babu DC!!
 
Sasa mkuu mbona unapotea tena? au toa contact basi umeanza vizuri sana malizia vizuri basi!!
 
Reactions: LAT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…