wa baha ela
Member
- Jan 20, 2013
- 37
- 5
Habari wapendwa!, ni mara ya kwanza kuandika chochote mahali hapa. Kikubwa naomba kufahamishwa kwa wale wenye uzoefu. Nina Diploma in Electronics and Telecommunicatrions Engineering kwa bahati nzuri nilipata ajira miezi mitatu baada ya kuhitimu. Nilikua nafikiria kujiendeleza kielimu kupitia Open Univ. of Tanzania huku nikiendelea na kazi. Je kuna uwezekano wa kupata mkopo kutoka board nikiomba kusomea ICT? Nilimaliza Diploma 2011. Changamoto yangu ni kwamba siwezi kuacha kazi sababu ajira ni ngumu af kujisomesha nayo ni ngumu kiasi sababu mshahara hautoshelezi. Nitafurahi kusikia chochote kutoka kwako. Asante Sana.