Mkopo wa Elimu ya Juu kwa Kila Muombaji

Mkopo wa Elimu ya Juu kwa Kila Muombaji

Umependa mbadala upi

  • Mbadala wa kwanza: Hali ilivyo sasa

    Votes: 4 17.4%
  • Mbadala wa pili: Hali ya sasa ikiboreshwa kidoogo

    Votes: 8 34.8%
  • Mbadala wa tatu: Sekta binafsi itoe mikopo

    Votes: 11 47.8%

  • Total voters
    23

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Nianze na kusema, nina shitariki ya mawazo ya udogo wa serikali (small Government), na, haki na wajibu kwa mtu binafsi (individual rights and responsibility); mawazo yanayoweza kujumuishwa kwa dhana ya Ruksa (Liberty).

Tuje kwenye mada.

Suala la mikopo ya elimu ya juu ni suala tete na mtambuka. Kwa baadhi ya waombaji, kukubaliwa kupata mkopo au kutokubaliwa kunamaanisha kupata elimu ya juu au kukosa. Hivyo basi, jitihada zimekuwa zikifanyika kuhakikisha kila mwombaji mkopo elimu ya juu anapata mkopo huo. Dhumuni la mada hii ni kuainisha njia mbadala za kufikia lengo hilohilo la mkopo wa elimu ya juu kwa kila mwombaji.

Mbadala wa Kwanza
Serikali ndio mwenye wajibu wa kuhakikisha kila anayetaka kwenda elimu ya juu anawezeshwa kifedha kwenda kusoma. Vyombo vya serikali ndivyo vyenye dhamana ya kukopesha. Navyo vinaweka masharti ya nani astahili kupata mkopo au kukosa. Wale wanaokosa, baadhi hutoa lawama kwa serikali. Rasilmali fedha zisingekuwa changamoto, kila mwombaji angepata kadiri anavyotaka. Huu mbadala ndio kwa kiasi kikubwa hali halisi ilivyo sasa. Mbadala huu unaegemea shitariki ya mawazo ya Ujamaa (socialism) kwa kuchukua hela kwa watu wengine (walipakodi) na kuzigawa, ngaa kwa mkopo, kwa watu wengine (waomba mkopo).

Mbadala wa Pili

Mbadala huu ni wa kubadili kidogo Mbadala wa kwanza. Waombaji mkopo wanawekwa kwenye mafungu, tuseme, manne.

(a) Fungu la kwanza la wasiohitaji mkopo kabisa. Vyuo vingekaribishwa kudahili wanafunzi walio na uwezo wa kujilipia kwa 100%. Nafasi, tuseme, asilimia 60 ya nafasi ziliopo zinatengwa kwa ajili hii.
(b) Fungu la pili la wanaohitaji mkopo kiasi, tuseme, kuanzia 0.1% mpaka 49% ya gharama za elimu ya juu. Hawa, tuseme wanatengewa asilimia 20 ya nafasi zilizopo. Awamu yao ya udahili inafuata baada ya ile ya kwanza.

(c) Fungu la tatu la wanaohitaji mkopo mwingi, kuanzia 50% ya gharama mpaka 75%. Hawa tuseme wanatengewa asilimia 10 ya nafasi zilizopo, na wanapewa fursa ya tatu ya udahili.

(d) Fungu la nne ni la wanaotaka mkopo 100% ya gharama au pungufu kidogo. Hawa wanapewa fursa ya mwisho kudahiliwa, na wanagombea nafasi zilizobaki.

Kila mwombaji kwenye awamu moja, hapati fursa ya kuomba mkopo awamu nyingine.

Mbadala wa Tatu
Katika mbadala huu, serikali inajitoa kwenye biashara ya kutoa mikopo ya elimu ya juu. Kila mwananchi anapewa wajibu wa kujigharamia elimu ya juu, na haki ya kuchagua mkopeshaji mwenye masharti anayoyaweza.

Serikali inatunga tu sera kuhusu masharti yanayoweza kutolewa, mathalan, mintarafu:
1. Muda wa mkopo
2. Kiwango cha riba
3. Masharti ya makato
4. Ukomo wa mkopo (e.g., nini kitatokea iwapo mkopaji atafariki au atatangaza kufilisika)
5. Mahitaji ya dhamana ya mkopo
6. Utaratibu wa kuzisarifu pesa za mkopo.
7. n.k.

Kwa njia hiyo, kila mhitaji wa mkopo wa elimu ya juu atajichagulia mkopeshaji, na kiwango cha kukopa, kadiri atakavyoona vema. Serikali itakuwa na jukumu la kutunga sheria za mchezo, huku refarii akiwa ni soko huria.

Serikali inaweza kuzihamasisha taasisi za kukopesha kwa kuziongezea mtaji au isifanye hivyo.

Katika mibadala hii mitatu, mbadala huu utakuwa ndio maridhawa zaidi kwani utakuwa unaiacha serikali ifanye kile inachofanya vizuri zaidi: kutunga sera, na kuachia sekta binafsi ifanye kile inachofanya vizuri zaidi: kufanya biashara; na mwisho wa yote kumwachia mwananchi fursa ya kufanya maamuzi binafsi.

Nawasilisha.
 
Serikali yoyote duniani ina wajibu wa kikatiba, kisheria na kiutendaji kuhakikisha inatoa huduma za jamii kwa 100%. Na hilo hasa ndio jukumu la serikali na ndio maana ya serikali. Huduma hizo ni pamoja na huduma ya afya kwa raia wake, ulinzi, elimu, miundombinu nk. nk. nk.
Lakini pia serikali katika kutekeleza wajibu huu inaweza kutafuta njia mbadala ambayo itaipunguzia serikali gharama lakini itahakikisha kila raia anapata huduma hizo pasipo kukosa.
Kwa mfano kwa huduma ya afya serikali inaweza ruhusu hospitali binafsi zinazoendeshwa kibiashara. Ili watu wenye uwezo watibiwe huko. Kwa kufanya hivyo serikali inafaidika kwa kuwa inapunguziwa mzigo wa kuhudumia watu. Lakini pia serikali lazima iweke hospitali za serikali kwa wale wasio na uwezo au kwa wale ambao hawajisikii kutibiwa hospitali binafsi.
Na yeyote anaetibiwa hospitali ya binafsi wakati wowote anaweza kutoka huko na kurudi hospitali za serikali bila maswali.
Maana yangu ni kuwa kila Mtanzania mwenye uwezo anastahili mkopo isipokuwa kama yeye mwenyewe hatahitaji. Hakuna haja ya kuanza kupanga mafungu huku ni kuwagawa watoto wetu vibaya. Ni kuligawa taifa. Watoto wote wanaosoma watakuja kulihudumia taifa bila ya kujali walisomaje. Wasomi ni fahari ya taifa. Tuiombe serikali iwapatie haki ya mikopo watoto wote isipokuwa wale ambao watasema hawauhitaji.
Kwa utaratibu wa sasa naona giza nene linajongea huduma yetu ya jamii (social services).
 
Serikali yoyote duniani ina wajibu wa kikatiba, kisheria na kiutendaji kuhakikisha inatoa huduma za jamii kwa 100%. Na hilo hasa ndio jukumu la serikali na ndio maana ya serikali. Huduma hizo ni pamoja na huduma ya afya kwa raia wake, ulinzi, elimu, miundombinu nk. nk. nk.
... (social services).

Serikali ya Mtaa ina wajibu gani kwa wananchi? Kwa nini serikali kuu itegemewe kufanya hayo yote? Nadhani kazi ya serikali ni kuweka mazingira mazuri kwa wananchi kujiletea maendeleo yao wenyewe. Pale inaposhindikana, basi serikali inaweka mkono wake kuokoa jahazi.

Maelezo yako yanaonyesha hupendi mbadala wa pili uliotajwa kwenye OP. Kwa hiyo unapendelea mbadala wa kwanza au wa tatu?
 
Back
Top Bottom