Mkopo wa kilimo

Mgengeli

Senior Member
Joined
Sep 23, 2011
Posts
193
Reaction score
13
wana jf naomba kujua mahali ninaweza kupata mkopo wa kilimo, nina hekari 50 zina hati ya miaka 30 na ziko eneo la wilaya ya kasulu mkoa wa kigoma,je ninaweza kupata mkopo wa kilimo? vikiwamo vifaa?,naomba msaada wenu
 
mkuu nenda TIB haraka sana!
 
Shukurani kwa ushauri wako umenifungua macho ubarikiwe
 
wana jf naomba kujua mahali ninaweza kupata mkopo wa kilimo, nina hekari 50 zina hati ya miaka 30 na ziko eneo la wilaya ya kasulu mkoa wa kigoma,je ninaweza kupata mkopo wa kilimo? vikiwamo vifaa?,naomba msaada wenu

TIB na mabenki mengine wanatoa mikopo ya kilimo.
Na kwasababu una hati ya shamba lako, ni rahisi sana kupata mkopo.

Kabla ya kuomba mkopo, kwanza andaa mchanganuo wa mradi wako huo wa kilimo (business plan).
Mchanganuo huo utakurahisishia yafuatayo:-
  • utaweza kufahamu kiasi cha mkopo unaohitaji
  • utaweza kuwashawishi kirahisi watu wa benki wakupe mkopo wakisoma mchanganuo wako
  • utaweza kufuatilia siku hadi siku matumizi ya pesa za mkopo katika kufanikisha vipengele mbalimbali vya mradi wako wa kilimo
  • utaweza kupima mafanikio yako kwa kulinganisha matokeo ya mradi wako wa kilimo na mipango uliyoiweka kwenye mchanganuo huo.
Kila la heri Mkuu Kutembea.
 
nashukuru sana je humu ndani kuna mtu anayeweza kuniandikia mchanganuo huo wa kilimo cha umwagiliaji na hasa mpunga?
 
Nilishawahi Kwenda TIB masharti yao bado ni magumu tu kwa mkulima mdogo niliambiwa shamba lako lazima liwe kuanzia ekari 500 na audited account statements za miezi sita iliyopita
 
Nilishawahi Kwenda TIB masharti yao bado ni magumu tu kwa mkulima mdogo niliambiwa shamba lako lazima liwe kuanzia ekari 500 na audited account statements za miezi sita iliyopita

mkuu hiyo ya ekari mia 5 si kweli mkuu labda ulienda kwa mhuni flani tuu, mie nimewahi enda pia hilo sharti sikuambiwa, ila lazima uwe na shamba!
 
mkuu hiyo ya ekari mia 5 si kweli mkuu labda ulienda kwa mhuni flani tuu, mie nimewahi enda pia hilo sharti sikuambiwa, ila lazima uwe na shamba!

Probably nilikuwa misled mkuu shamba la ukubwa gani walikuwa wanataka?
 
mkuu hiyo ya ekari mia 5 si kweli mkuu labda ulienda kwa mhuni flani tuu, mie nimewahi enda pia hilo sharti sikuambiwa, ila lazima uwe na shamba!

Hebu tusaidie mkuu, masharti yakoje?
 
Probably nilikuwa misled mkuu shamba la ukubwa gani walikuwa wanataka?

Mkuu sikuambiwa ni shamba ukubwa gani ila nilichoambiwa mikopo yao huwa wanatoa mikubwa tu kuanzia milion 100! kama upo dar nenda pale mlimani city utapata maelekezo mazuri na vipepelushi vyao kibao!
 
Hebu tusaidie mkuu, masharti yakoje?

mkuu ukweli ni kuwa lazima ujiandae vya kutosha ila mikopo ipo mkuu kama upo mikoani wanamatawi yao kila kanda.
niliambiwa natakiwa niwe na shamba na processing industry. mfano unaweza kuwa mkulima wa alizeti na ukawa na mashine ya kukamua mafuta ukawasaidia hata wakulima wadogo kwenye kununua alizeti zao. ukitaka kuongeza mtaji ndo watakupa mkopo tena kwa asilimia 5 ya interest marejesho ni kuanzia miaka 3. mkuu zaidi onana nao wenyewe wanamaelezo mazuri sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…