Mkopo wa matrekta -farm track tractor

FADHILIEJ

Senior Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
132
Reaction score
18
Wadau tafadhali mwenye taarifa kuhusu mikopo ya matrecta ya FARMTRACK tafadhali anijulishe,taarifa nilizo nazo ambazo hazina uhakikia ni kuwa yanauzwa milion 16 na ukitaka kukopa unalipa 50%.

mwenye taarifa sahihi atujuze tafadhali,bila kusahau utaratibu na wapi zinapatikana.

nawasilisha

asanteni
 
Nenda Suma JKT, viambatanisho muhimu ni barua ya muajiri au mdhamini anayeaminika, barua ya mwenyekiti wa mtaa, kitambulisho, na kadi ya CCM iliyolipiwa hadi mwaka 2012.
 
mmmmh!! Mjepu hiyo kadi nikiwa nayo ya CHADEMA lakini sijailipia vipi!!!
 
Last edited by a moderator:
mmmmh!! Mjepu hiyo kadi nikiwa nayo ya CHADEMA lakini sijailipia vipi!!!

Ofisi zao zipo pale Lugalo kwenye kambi ya jeshi, ukienda na kadi yako ya CHADEMA ujue badala ya kurudi na trekta utarudi na upungufu wa korodani mwilini ( UKOMWI)
 
Ofisi zao zipo pale Lugalo kwenye kambi ya jeshi, ukienda na kadi yako ya CHADEMA ujue badala ya kurudi na trekta utarudi na upungufu wa korodani mwilini ( UKOMWI)
mmmh!huko sitii mguu wasije wakaninyofoa kucha!!
 
[asante kwa ushauri,ila mbona mambo ya siasa tena? madQUOTE=Mjepu;5613401]Nenda Suma JKT, viambatanisho muhimu ni barua ya muajiri au mdhamini anayeaminika, barua ya mwenyekiti wa mtaa, kitambulisho, na kadi ya CCM iliyolipiwa hadi mwaka 2012.[/QUOTE]
 
mkuu ni vizuri tukapeana tarifaa za ukweli, bei ya trecta dogo bila jembe ilikuwa 19,600,000/= hp 60 unalipa kama milioni 6 unapewa trecta kwa mwaka inatakiwa ulipe installment 4 muda wa mkopo miaka 3 hadi 4, hp 70 ni milioni 29 unalipa kama millioni 9 VIAMBATANISHO hati ya nyumba kwa wenye nyumba , wasio na nyumba barua ya utambulisho kutoka serikali ya kijiji kuonyesha unashamba pamoja na kupitishiya maombi yako ofisi ya kilimo wilayani. KWA SASA MATRECTA YAMEKWISHA WANASEMA WALETA TENA MAY AU JUNE 2013
 
Nenda wizara ya Kilimo na Mifugo..Kwa mujibu wa wizara ya kilimo.... miliki eneo hata kwa hati ya kimila...popote tanzania.... nenda na barua ya maombi ikiambatanishwa na nakala ya hati husika.. Wizara ina mkataba na makampuni kadhaa yanatoa mkopo wa matrekta na mafuzo ya kitaala na huduma za ukarabati... kama sijasahau mkopo unaanza rejeshwa kuanzaia miaka 3...!!
 

This sounds good, lakini kama kuna kitu kizuri kama hiki mbona haitangazwi sana au haivumi kabisa?
 
This sounds good, lakini kama kuna kitu kizuri kama hiki mbona haitangazwi sana au haivumi kabisa?

hili tatizo sugu kwa taasisi za serikali... hawapendi kutangaza huduma/fursa kupitia vyombo vyetu tulivyozoea... hadi uwatembelee ndo utajifunza... sielewi ni kubweteka au wanafanya chinichini wanufaike wachache.. binafsi niliwatembelea bandani kwao kufaham machache haya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…