Mkopo wa Mfadhili waanza kuliwa Chalinze

Mkopo wa Mfadhili waanza kuliwa Chalinze

Richard Robert

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
632
Reaction score
340
Leo Watanzania mnasherekea mkopo wa IMF na kufurahia maekekezo tu kuwa tunakwenda kumaliza tatizo la vyumba vya madarasa na wasimamizi ni wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya chini na watendaji. Lakini tujue maeneo mengi ya nchi yamejaa upigaji. Na wapigaji ni wasimamizi wenyewe.

Shida ipo hapo Halmashauri ya Chalinze kata Bwilingu, kitongoji cha Bwilingu shule ya msingi kibiki walipata mfadhili anawajengea vyumba viwili vya madarasa na ofisi ambazo inategemewa na wananchi.

Timu ya wasimamizi wa mradi imeamua kumlipa kada wa CCM pesa ya kifusi 80000 kwa Kila gari na wakati wanatambua Bei ya soko ni 50000 na waliambiwa wakaziba masikio. Pia tuna taarifa kuwa hata hela ya mradi imeshapigwa tayari.

Sasa je katika mazingira haya Si ni kiini macho tu wasimamizi ndio wapigaji? Je, miradi ya IMF SI ITAHUJUMIWA KILA KONA?
 
Nchi hii kuna msemo maarufu wa "KILA MBUZI ......."
 
Leo Watanzania mnasherekea mkopo wa IMF na kufurahia maekekezo tu kuwa tunakwenda kumaliza tatizo la vyumba vya madarasa na wasimamizi ni wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya chini na watendaji...
Ni vizuri umetanabahisha. Wakubwa watafuatilia na kila aliyehusika atawajibishwa.
 
Mkuu hongera kwa kuwa mzalendo ila kama umewachoma wezi wenzio kwa kuwa umenyimwa ulaji Mungu akushughulikie.
 
Back
Top Bottom