"Mkorogo Umenitia Adabu sana na kuniaribia ngozi yangu nzuri ya awali...Wema Sepetu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
MISS Tanzania 2006 aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa, mkorogo umemtia adabu na anajuta kuutumia mwilini mwake.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Wema Sepetu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
.
Akizungumza juzi na paparazi wetu ofisini kwake jijini Dar, Wema alisema kuwa baada ya kwenda kliniki nchini China na kupata matatibu ya ngozi yake ambayo sasa imerudi kama mwanzo amejifunza kitu.
NI KITU GANI HICHO?
Wema alisema amejifunza kuwa, binadamu anatakiwa kuishi alivyoumbwa na Mungu, mambo ya rangi ya mwili hayana nafasi katika uwezo wa binadamu.
ALIAMINI USTAA NI LAZIMA UWE MWEUPE PEE!
Wema akatoa mpya zaidi aliposema kuwa, uamuzi wake wa kutumia mkorogo ili awe mweupe kama mzungu (yeye ni mweupe) ulitokana na kuamini kwamba, weupe na ustaa ni mambo yanayokwenda pamoja, kumbe sivyo.
“Niliamini weupe sana na ustaa ni Kulwa na Doto, lakini sivyo. Ngozi yangu ya awali ni nzuri, imerudi kama ilivyokuwa, namshukuru sana Mungu,” alisema Wema.
AWAONYA MASTAA WENZAKE
Akiendelea kuzungumza na paparazi, Wema alitoa ujumbe kwa mastaa wenzake wanaotumia mkorogo kuwa, hakuna faida yoyote, kwa sababu mkorogo unaondoa vitamini yote mwilini.
“Daktari kule China aliniambia kuwa licha ya kupoteza vitamini nyingi mwilini, pia mkorogo unakufanya mtu uzeeke kabla ya wakati. Mimi nawaomba kabisa mastaa wenzangu wajiepushe na hii kitu inaitwa mkorogo,” alisema Wema.
ALICHOJIFUNZA KUHUSU KUJIKOBOA
Kujikoboa ni kuwa mweupe sana, lakini Wema anasema alichojifunza kuhusu hali hiyo ni kwamba, ni rahisi sana kuiondoa ngozi ya awali kwa mkorogo lakini inapofika ngozi ya awali inatakiwa kurudi inagharimu sana.
“Ukitaka kuona maajabu sasa, ngozi yako mwenyewe kuibadilisha si kazi na wala si gharama lakini ukitaka irudi kama mwanzo ni lazima ugharimike sana, mimi sitaki tena jamani,” alisema Wema.
 
wadada natumaini watajifunza kutoka kwa wema na wataacha kujiingiza kwa mkorogo
 
hongera kuwa kungwi wa wadada kwakweli unawafaa sana

wewe endelea kupaka mkorogo wako ipo siku utakuja kusimulia. naona nimekugusa adi umekasirika. pole sana ila uache mkorogo si mzuri
 
Si alisemaa mpaka maduka yafungwe ua vipodoz leo ameyageuka hahahshahahahahshagahahss
 
zoezi la ufukuaji makaburi linaendelea tunaomba ushirikiano
wenu wakuu
 
Airbus nyingine inatua kesho. Tukaipokee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…