Tusimkatishe tamaa mkubwa fela,amewekeza kwenye muziki pia inabidi na wenyewe umlipe, wale yamoto kukosa fela wasingeweza hata kufanya chochote,fela amewajengea nyumba pia amewapangishia nyumba amelipa milioni 12 kwa mwaka mzima.
Ukitaka kumuelewa fela kuna wimbo wake aliutoa unaitwa 2008 eheee 2009,amezungumza sana haya madai:-
1.Umekuja na ndala unaondoka na gari.
2.Ulikuwa unalala sebureni sasa umeondoka na nyumba.
3.Ulikuwa unaombaomba hela ukichungulia bank na mfuko imetuna.
4.Ulikuwa unashindia kahawa hivi sasa Milo yote unaipata.
Sasa hapa nani anadhulumiwa? Fela nachomlaumu ni kwenye uhusiano wake na OSATA tu na figisu figisu zao.